Hii ni aibu sana: Haiwezekani mtu akaulizwa kuhusu uvutaji wa hewa ya Oxygen akasema ni kitu kibaya

Hii ni aibu sana: Haiwezekani mtu akaulizwa kuhusu uvutaji wa hewa ya Oxygen akasema ni kitu kibaya

Remark

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2015
Posts
510
Reaction score
989
Hii clip ya video inazidi kudhihirisha wazi kabisa Watanzania wengi hawana elimu kama tu mtu anaulizwa swali linalomzunguka kwenye mazingira yake lakini anachojibu ni vitu viwili tofauti.

Kiukweli mpaka nimejisikia aibu sana kutokana hili.

Kiukweli hakuna taifa lolote lililoendelea au linalotegemea kuendelea likiwa na aina hii ya watu Kama serikali haitakabiliana na situation hii Basi tunasafari ndefu mno
 
Attachments

Naomba niungane na wewe kuonyesha masikitiko yangu, ila atakae itazama hio video asisite kutuelezea madhara ya kuvuta oxygen ili tuendelee kusikitika zaidi.

Maendeleo hayana chama
Mimi ninawasikitikia nyie kwa kusikitika kwenu lakini pia nasikitika sijaangalia hio video

mvujajasho nguli
 
Hii clip ya video inazidi kudhihirisha wazi kabisa watanzania wengi hawana elimu Kama tu mtu anaulizwa swali linalomzunguka kwenye mazingira yake lakini anachojibu ni vitu viwili tofauti. Kiukweli mpaka nimejisikia aibu sana kutokana hili.
Kiukweli hakuna taifa lolote lililoendelea au linalotegemea kuendelea likiwa na aina hii ya watu Kama serikali haitakabiliana na situation hii Basi tunasafari ndefu mno
Kuna dada kamaliza digrii ya sanaa kaniambia hajawahi kununua gazeti wala kusoma gazeti lakini ana uwezo mkubwa sana kufuatilia umbeya wa magroup kadhaa ya whataspp, hajui waziri wa ulinzi ni nani lakini anaweza kuimba nyimbo za Diamond platnumz zote. Elimu yetu ni janga la taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ninawasikitikia nyie kwa kusikitika kwenu lakini pia nasikitika sijaangalia hio video

mvujajasho nguli
Hayo masikitiko yako yamenisikitisha mpaka mimi, ila kabla ya kutusikitikia sisi kwa kusikitika kwetu na sisi pia tunakusikitikia sana tena kwa masikitiko makubwa kwa kutoitazama hio video jinsi inavyosikitisha.

Maendeleo hayana chama
 
Kuna dada kamaliza digrii ya sanaa kaniambia hajawahi kununua gazeti wala kusoma gazeti lakini ana uwezo mkubwa sana kufuatilia umbeya wa magroup kadhaa ya whataspp, hajui waziri wa ulinzi ni nani lakini anaweza kuimba nyimbo za Diamond platnumz zote. Elimu yetu ni janga la taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Asilimia kubwa ya wanachuo katika vyuo vya Dsa(institute of accounts) na Cbe matawi yote wanaochukua digrii ni form four waliopata division four. Hakuna form six aliyefaulu vizuri anayeomba kusoma vyuo hivyo fikiria products zikoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Kenya na Uganda wamefanya hizo clips na matokeo ni hayohayo .... Kuhusu suala la uelewa inategemea na aina ya watu unaokutana nao
 
Kwa Kiswahili inaitwa aje? Hii tabia ya wanaohoji kutumia neno moja la Kiingereza kuchanganya watu haifai. Shule ya msingi tulielezwa hewa safi, licha ya kuwa oksijeni pia lilitumika ila, nyumba bora ilitakiwa kuwa na vitu mbali mbali ikiwamo uwezo wa kuingiza hewa safi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom