Hii ni aibu, uzinduzi wa miradi isiyokamilika

Hii ni aibu, uzinduzi wa miradi isiyokamilika

Baraka21

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2021
Posts
1,262
Reaction score
3,184
Maana ya uzinduzi ni pale mradi unapoanza au pale ulipokamilika.

Ni aibu Rais kufunga safari kwenda kufanya uzinduzi wa maji ya bilioni 17 Longido halafu unasema kufikia Januari 2022 mtapata maji, kwanini usisubiri Januari ifike ukazindue kitu kilichokamilika?

Huo mradi wa Arusha wa bilioni 510 umezinduliwa zaidi ya mara 3 kabla ya kukamilika. Haraka ya nini kwanini msisubiri miradi ikamilike ndio mkazindue?

Acheni kuchezea kodi za wananchi na zinduzi feki.

Mwendazake baada ya kukosa kazi akawa anazindua hadi miradi ambayo ilishazinduliwa tayari mfano barabara ya Tunduma- Sumbawanga. Tafadhali awamu ya 6 msiige huu ujinga.
 
Miradi ni mingi raisi akipita sehemu kama kuna mradi unaelekea kukamilika na kama mradi ni wa hadhi yake , anauzindua Tu mana anaweza asipate mda wa kuuzindua pindi utakapokamilika
 
Miradi ni mingi raisi akipita sehemu kama kuna mradi unaelekea kukamilika na kama mradi ni wa hadhi yake , anauzindua Tu mana anaweza asipate mda wa kuuzindua pindi utakapokamilika
Sawa mkuu
 
Miradi ni mingi raisi akipita sehemu kama kuna mradi unaelekea kukamilika na kama mradi ni wa hadhi yake , anauzindua Tu mana anaweza asipate mda wa kuuzindua pindi utakapokamilika
Tumekusikia polepole!
 
Back
Top Bottom