SI KWELI Hii ni akaunti rasmi ya Mtandao wa X ya Mbunge wa Kisesa Joelson Luhaga Mpina

SI KWELI Hii ni akaunti rasmi ya Mtandao wa X ya Mbunge wa Kisesa Joelson Luhaga Mpina

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa na akaunti yenye jina la Luaga Mpina inachapisha taarifa mbali mbali kuhusu mambo yanayoendea nchini na kujibu hoja za Mbunge Luaga Joelson Mpina wa jimbo la Kisesa ndani ya mtandao wa X zamani twitter.

Naomba JAMIICHEK inisaidia kujua ukweli kama akaunti hii ni mali halali au inamilikiwa na Luaga Joelson Mpina mwenyewe ambaye ni mbunge wa jimbo la Kisesa na kwa sasa yuko nje ya bunge kwa adhabu.

Screenshot_20240912_111339_X.jpg
 
Tunachokijua
Luhaga Joelson Mpina ni mbunge wa jimbo la Kisesa katika bunge la Jamhuri ya Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi(CCM)
Luhaga_Mpina.jpg
Kuna akaunti zimejisajili kwenye mtandao wa X moja kama Luhaga Mpina na nyingine Luhaga Joelson Mpina ambazo moja iliyoandikwa Joelson Luhaga Mpina imeandika kwenye utambulisho wa akaunti ya X(Bio ya mtandao wa X) kuwa ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambayo akaunti hii ilijiunga mtandao Oktoba 2017 kwenye wa X zamani ukijulikana kama Twitter.
1726208923946-png.3094699

Ya pili iliyoandikwa Luhaga Mpina imeweka utambulisho kwenye(BIO ya mtandao wa X) kuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, akaunti hiyo ilijiunga kwenye mtandao wa X Julai 2024.
1726209213980-png.3094702

Je, ni kweli akaunti hizo ni za Joelson Luhaga Mpina Mbunge wa Kisesa?

Jamiicheck
imetafuta kufahamu iwapo akaunti hizo ni za Mbunge wa Kisesa, Joelson Luhaga Mpina na kubaini kuwa akaunti hizo Si za Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina kwani Agosti 25, 2024 alipokuwa Mwaukoli, Jimbo la Kisesa akizungumza na Wananchi wa Kisesa alikanusha kuwa hana akaunti yoyote kwenye mitandao ya Kijamii.

Kwenye Mitandao huko ya Kijamii, Mpina anazuliwa mambo mengi sana, kwanza nataka niseme mimi sina akaunti kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu zangu binafsi ninazozijua, kama mbunge wenu sina akaunti yoyote kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu zangu binafsi ninazozijua, sasa hivi karibuni kuwa watu wamefungua akaunti na kusema hiyo ni akaunti ikafunguliwa kwa jina Luhaga Mpina, na wakaweka picha ya Luhaga Mpina, na wamekuwa wakiongea maneno yao, wakiandika mneno yao kwenye mitandao hiyo kwamba iripotiwe kwamba ameandika Luhaga Mpina.

Nataka kusema kuw mimi sina akaunti yoyote kwenye mitandao ya kijamii, kwa sababu nazozijua mwenyewe, Mimi nikitaka kuishauri Serikali nashauri sikimbiagi kushauri kwenye mitandao, huwa nasimama hadhrani kusema hivihivi nachotka kusema kwa Serikali, nikiwa ndani ya Bunge nikitaka kumshauri Rais namshauri Rais kwa wazi na kwa jina lake.

Nikitaka kumshauri Waziri Mkuu, namshauri kwa jina lake, kwa sauti na sura yangu inaonekana, siendagi kuandika kwenye mitandao, kwa hiyo hayo yanayondikwa kwenye mitandao yapuuziwe, lakini niwashauri Watanzania ukitaka kuishuri Serikali wewe ishauri tu kwa nini mpaka utumie jina la mtu mwingine, kama unaushauri wko mzuri unataka kuishauri serikali wewe ishauri tu kwa hiyo nadhani wamesikia na wameelewa na waache utaratibu huo na hiyo akaunti ifungwe.
Alisema Luhaga Mpina(Tazama video ya kanusho)

Aidha, JamiiCheck iliwasiliana na Mbunge wa Kisesa ambaye alithibitisha kutokuwa na akaunti yoyote kwenye mtandao wa X(Tittwer)

Sina Akaunti yoyote Twitter. Mtu kama anataka kuishauri Serikali atumie jina lake mwenyewe sio la Mpina.
Back
Top Bottom