Hii ni CCM toleo la 4 na la mwisho; hakuna CCM nyingine baada ya hii!

Hata yeye anayaona na kuyajua madhara ya katiba mpya kwa upande wake, anajua hawakushinda, ukijumlisha na katiba mpya ndio kwa heri kabisa.
 
Angalia idadi ya wabunge, maDC, maRC, DAS, DED na RAS waliokuwa upinzani sasa wapo ndani ya CCM. Kutakuwa na wanaccm wapinzani ndani ya CCM yenyewe. Subiri muda utaongea wacha mimi niendelee kuota ndoto za mchana nikiamka itakuwa usiku
Ona huyu anaota mchana. [emoji23]

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna upinzani uliojiandaa kuitoa CCM madarakani. CCM ya sasa sio chama tena bali ni taasisi.

Nimeshuhudia CCM ikifanya vikao mchana na usiku kupanga mikakati ya kuendelea kutawala.

Wakati vyama vya upinzani vipo bado kiharakati, CCM ni taasisi inayoendelea kukomaa kila kukicha.

Wananchi ambao hawaipendi CCM wanashindwa kuchagua chama mbadala nje ya CCM kwa maana hawaoni sera wala ajenda mpya za upinzani zenye tija. Hivyo hawapigi kura au wanaamua kumpigia kura mgombea wa CCM.

CCM itaendelea kutawala mpaka pale itakapo sambaratika yenyewe.

Huo ndio ukweli mchungu.
 
CCM itaendelea kutawala mpaka pale itakapo sambaratika yenyewe.!!¡!
Na kusambaratika huko kumetimia.. Kwakuwa ccm ya sasa ni zaidi ya kachumbari..maana mpaka vinegar imo
 
Unasikitisha mkuu. Inaonesha haujui hata tofauti ya chama na serikali. Hao unaowaita wapinzani hawana mizizi wala ushawishi wowote ndani ya CCM.
 
Mpaka sasa hakuna upinzani unaoweza kuitoa CCM madarakani. Haupo.
Mwaka 2021 chama cha mapinduzi kiliwatumia TISS, polisiccm, DED nk kupiga kura siku moja kabla ya uchaguzi. Mfno pale ofisi za ccm kinondoni vijana waliitwa na kupiga kura za ndiyo kwa ccm na wagombea wake wote waliahidiwa 5000/ hawajapewa mpaka leo.
Kule kasulu haya yalifanyika kwenye jumba la maendeleo. Kwinginepo wasimamizi wakuu waliamriwa kuingia na kura saa 9 usiku.
Haya siyo maneno ya kufungwa nimejionea na kuongea na walioshiriki zoezi hata yule mwendazake kutangaza mshindi
 
Kama hauwezi kuithibitishia mahakama, unaongea porojo tu.
 
Kama hauwezi kuithibitishia mahakama, unaongea porojo tu.
Mahakama hizo zinazoundwa na wana ccm? Wewe ndiyo unaongea promo kama hata haya hukuyaona na kusikia. Huko kwenu namtumbo hakukuwa na wizi wa kura?
Tume ya taifa siyo huru.
Kimuundo
Kinadharia
Matendo.
Kabla ya uchaguzi mkurugenzi wake alisikika akimpangia mgombea wa upinzani mambo ya kuongea kwenye kampeni zake. Mfno watu anataka kusikia sera juu ya maji, elimu no na siyo matusi .... badala yake akamuacha yule kichaa mwendazake atukane wenzake kwa Kuwait's wanaounga mkono mashoga! Kama haya hukuyasikia siyo jukumu langu kuthibitisha
 
Kama hauwezi kuthibitisha hauna haki ya kuongea chochote.
 


chadema + ACT
 

uchaguzi umeisha dogo, chapa kazi mlete mgombea mwingine tumpe kifinyo
 
Hana hata miaka miwili umeanza kuongea hivi unajuaje akija bugi mbele kama mwendazake ww ndo utakuwa wa kwanza kulaumu. Tunakuhifadhi for future reference
 
Kama hauwezi kuthibitisha hauna haki ya kuongea chochote.
Kwakuwa wewe ni miongoni mwa.wanufaika wa mfumo ndo mana unataka ithibitishwe hapa. Haishangazi kusikia mgombea amewekewa pingamizi au kuondolewa kabisa ati kwakuwa ameandika jina kwa herufi ndogo/kubwa na upuuzi unaofanana na huo rejea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019. Matokeo yake huko TANDIKA CCM imempitisha jambazi kuwa mkiti wa mtaa.
 
uchaguzi umeisha dogo, chapa kazi mlete mgombea mwingine tumpe kifinyo
Umpe kipigo kwakuwa unategemea hao wapuuzi hapo makumbusho?
Kwakuwa unawahonga waandishi wa habari kuwapa UDC ili ukamate news room?
Unategemea kina mambo sasa useme unamgagaza mtu?
Embo twambie sasa kama kweli ulishinda pale kinondoni ccm wale vijana walipiga zile kura walimpigia nani?
Unafikiri sisi hatujui au hatuishi duniani????
 
Nashukuru kuota mchana kumeruhusiwa tangu mwanadamu alipotoka Eden.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…