hii ni kawaida jamani??

NILHAM RASHED

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
1,622
Reaction score
43
s. aleykum... akhbar zenu jamani niliwatupa kidogo vp mambo zenu? my hope ua all doing okay.... mi nna swali la kirafiki tuu....nimeona bara niiulize hii hal na vipi niiepuke....
ni kwamba yaani kila ikifika birthday yangu nnakuwa mnyonge na mwenye kulia na sababu siijui na sana sana mosst of dah time wallah anakuwa ni mama ndie anetawala mawazo yangu,,, na hakuna anaenifurahisha kwa siku ile ya part ispokuwa yeye na hata kama nikiwa kwenye hali ile ya majonzi yeye anambiapo happy birthday basi najiona hakuna alienipa zawadi kama yeye japo ni ya maneno huwa naridhika...

yaani hali hii wallah yanikosesha raha kwa ajili part nitaiandaa week nzima then nashindwa kuifurahia ni kwanini?? na hal hii huwa inatokea kwa wengine au vipi.... na ni vipi niepukane nayo??
 
Karibu tena dia'
Ohoo pole sna ila hakuna kama mama duniani. Tusubiri michango ya wengine
 
oopppsss:A S 13:... i'm here again with u ... thats why i like u sooo much.... then shukran...
Karibu tena dia'
Ohoo pole sna ila hakuna kama mama duniani. Tusubiri michango ya wengine
 
Love you too my dia
Nilikumiso kweli kweli... tuendelee na topic ya mama imenigusaaa
 
Labda unakuwa na huzuni kwa sababu kadri unaposherehekea Birthday umbali kati yako na mvi unazidi kupungua?

:rain:
 
duh....
kaone psychologists hapo...vingine nitakuwa nakudanganya tu!
 
Pole sana huwa inakuwa hivyo mie huwa nashindwa hata kunywa soda hata keki niliyoandaa mwenyewe
 
Pole sana my dear.....its kind of natural....the most happiest days of my life waga nalia....nakumbuka mema na mabaya yote yakiyowahi nikuta....nashukuru tu siku hazigandi,nikiamka asubuhi ya kesho yake,nakuwa kawaida.....umeshajua una tatizo hilo,sasa ikifika siku ya birthday...unajitahidi ku cheer up.....halafu mimi na mama yangu tuna connection strange,nikiwa na maumivu ya kimwili au kiroho bila hata kumuambia,atapiga simu kuuliza hali yangu na kusema hajisikii vizuri na anahisi nina tatizo....hata nikimdanganya,the next day atapiga simu na nitasema ukweli then anasema roho inatulia kuujua ukweli......:hand:
 
pole na karbu tena ila jitahd kulia ni part of life haijalish unalia kwa baya au zur zoea
 
the way u said is what i have my dear.... nikianka asubuh yake nishasahau yaliopita ..... kumbe basi ni kawaida nishapata watu wawili wakanambia ni hali inayokuja automatically kwa yeyote anaejali mama na kumpa mapenzi yote...mh ok bas mwenzio nashindwa kunywa juic najua labda kuna dawa ntapewa na jf hii hali iniondokee kumbe ni kawaida sasa nisingeuliza ningejuaje...thanx my dear...
 
heehhh mie kulia kawaida yangu hata traffic ikiwa kubwa njiani nalia...tena ukute ndio natoka kazini nikikutana na hiyo traffic utanionea imani wallah..
pole na karbu tena ila jitahd kulia ni part of life haijalish unalia kwa baya au zur zoea
 

Take it easy my dear,sometimes you have to cry and when you have to....just cry and then life goes on!!!
 
heehhh mie kulia kawaida yangu hata traffic ikiwa kubwa njiani nalia...tena ukute ndio natoka kazini nikikutana na hiyo traffic utanionea imani wallah..
sasa watu ndo wanakukuta unamwaga machozi huko kwenye foleni,wanakuuliza mama vipi!!!unawajinuje sasa?
 
Jitahidi ifikapo siku yako kuzaliwa basi 'funga sunna', na ikibidi jitahidi siku 3 kabla ya birthday yako 'funga na zingatia ibada' kwa karibu saana. Hii ni ishara za shukrani njema kwa muumba wako.
LANGU: Katika hali za kiuchamungu...machozi huwa ni sehemu ya imaan ya mwaminio, zingatia.
 

Tatizo kubwa ni hilo (in red). Bila kujua sababu ya jambo, ni vigumu kupata ufumbuzi wake.

Kwa kweli, si kuwa sababu huijui sababu, bali usichokijua ni njia tu za kuifukua hiyo sababu. Moja ya njia hizo ni "kujitambua (self awareness)". Hili linahitaji maelezo marefu lkn ngoja nikushauri hivi: Kaa peke yako ktk sehemu ambayo kwako ni tulivu sana; ambayo hutapata bughudha yoyote -- vizuri ikiwa ni chumba kitupu au kisicho na samani (furniture) nyingi. Weka stool au kiti ktk kona mojawapo mbali nawe. Kisha mweke NILHAM ktk stool/kiti hicho. Sasa anza kumchunguza NILHAM kwa undani, historia yake tangu utotoni, maisha yake mtaani, shuleni, n.k., mambo anayoyapenda na asiyoyapenda; kwa kifupi, everything about her. Kubwa zaidi, chunguza udhaifu wake (huna la kuficha kwa sababu upo wewe, kivuli chako -- NILHAM in qn -- na Mwenyezi Mungu; wote hao hawawezi kutoa siri zako). Mtafiti pia NILHAM ili uweze kujua utatuzi wa kila tatizo na kikwazo. Ukiwa mkweli kwa NILHAM utajua mengi mno kumhusu yeye, na hivyo utajua pia njia za kutatua matatizo yake na kufukua uwezo na vipaji vyake.
 
Katika tamaduni za western China sherehe ya kuzaliwa uwa ni sawa sawa na msiba - Wao wanaamini kuwa unakaribia kufa (right?)...

Birthday inakuwa siku ya kukufariji ku-accept death!
 
duh....
kaone psychologists hapo...vingine nitakuwa nakudanganya tu!

Ni wazo zuri, lkn bila kuwa muwazi kwa mtabibu, ni vigumu mtabibu kukusaidia. Hivyo, ni vema mtu kuanza kuwa muwazi kwa nafsi yake mwenyewe km nilivyomjibu Nilham hapo juu.
 

Hapo umepata liwazo, hujapata ufumbuzi.
 

Michelle, kufanya hivyo (in red) ni kujaribu tu kuficha ukweli. Most of the time positive thinking doesn't solve a problem!
 


Kwa kawaida, watu ambao wanaweza kumfurahisha mtu katika siku kama hiyo ni, mama, baba, mlezi, ndugu, MPENZI, rafiki. Je, kati ya hao, zaidi ya mama, yupi pia anahusika na birthday yako (ambaye anakuwa karibu kwa wakati huo)?
Pili, raha ya birthday usijiandalie, tena usiihangaikie. Kaa kimya endelea na shughuli zako, alafu subiria surprise kutoka kwa mmoja kati ya hao waliotajwa hapo juu.
Tatu, kama umri wako unaruhusu kutokana na tamaduni zenu, then MPENZI ndiye atakayekufurahisha zaidi kuliko mama (maana unajisikia kuwa huyu nitakuwa naye hadi siku ya kufa). Kama anakuwa hayupo, na umeshakuwa mkubwa fulani, inatia simanzi na tena usipende kushrehekea birthday ikiwa hivyo.

Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…