Hii ni kemikali hatari iliyomo kwenye plastic

Hii ni kemikali hatari iliyomo kwenye plastic

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kwenye plastic kunakundi moja la kemikali linalipatikana kwa wingi ndani yake. Linaitwa biphenols. Hii ni kemikali hatari sana sababu ni carcinogenic. Na mbaya zaidi kemikali hii inafanana na hormone inayopatikana kwa wanawake iitwayo estrogen na inaweza fanya kazi za estrogen.

Hii inaweza fanya mwanaume kuwa tasa na kuharibu afya ya uzazi ya mwanamke. Wenzetu wamepiga marufuku chupa za watoto za kunyonyea maziwa zilizo na plastic za kuwa na hii kemikali.

Kwa sisi ambao matumizi ya vikombe na sahani za plastic ni makubwa kupita kiasi tutakuwa tuna mabiphenols kiasi gani mwilini mwetu? Ni vyema serikali ikapiga marufuku matumizi ya plastic kama vyombo vya chakula ili kulinda afya ya raia wake.
 
Kwenye plastic kunakundi moja la kemikali linalipatikana kwa wingi ndani yake. Linaitwa biphenols. Hii ni kemikali hatari sana sababu ni carcinogenic. Na mbaya zaidi kemikali hii inafanana na hormone inayopatikana kwa wanawake iitwayo estrogen na inaweza fanya kazi za estrogen. Hii inaweza fanya
Mkuu kama hili limethibitika kweli basi ni zaidi ya hatari hapa kwetu
 
 
Mkuu kama hili limethibitika kweli basi ni zaidi ya hatari hapa kwetu
Limethibitika na data zipo kibao. Makampuni ya plastic ili kulinda biashara zao yakaja na research zao mbadala wakisema kuwa biphenols hazina madhara kwa dozi ndogo.
 
Back
Top Bottom