mwakani naolewa
Senior Member
- Jul 25, 2024
- 148
- 426
Kwa wanawake wote wajasiriamali wafanyabiashara na wengine walojipata ,mwanaume yeyote akija kukufata kukutongoza ukamuelewa ukaona kabisa maisha yako yanakwenda kubadilika kupitia huyo mwanaume, ukaona kabisa huyu ni mwanaume wa ndoto zako, ukaona unayo ahidiwa ni mengiii na makubwaa. Naomba uwe na tabia ya kuingia google na kusearch majina ya hao wanaume na tabia zao kama Joel,Juma,Hashim whatever, tafuta kwenye social media hao watu fanya uchunguzi sana kuhusu hao watu. Najua tunafatwaga na watu wengiii sana wanaotuambia wameona kitu ndani yetu, wameona juhudi zetuu, wanataka ku invest sana kwetuu whatever, BE CAREFUL sana na hao watu wengi ni waongo sana. Kuna wanawake wengi sana wamedanganywa na hawa wanaume na wameishia kufilisiwa, kuibiwaa, kutapeliwa, kudhulumiwa kwa kigezo cha kusema watatuendeleza kibiashara, mara wanataka kutuongezea mitaji whatever, Matapeli haoo kua nao makini na uwachunguze sana.Tafuta taarifa za uyo mtu ulizia taarifa zake ulizia kwa watuu. kama kakwambia anafanya kazi sjui ofisi za TRA uliziaa kama kweli yupo uko, chunguzaa. dunia imeharibika wanaume wanatutapeli kwa kutuona sisi wadhaifu tunapenda kupendwa