Hii ni kwangu tu kuna wengine huwatokea???


Sijui kama umenielewa sio kwamba namshuku inatokea tu unasikia hivyo but akimaliza kuongea ama kuondokana nae yanakwisha hapo hapo si kwamba naendelea nayo hapana its just like that ndo maana nikasema si naona wivu anyway naweza kusema sipendi
 

Kama WIVU NI DHAMBI Mungu asingekua mwenye WIVU!!
 
Dena wala sikushangai ,mie huwa na wivu sana sema mara nyingi huwa najifanya sijaona kilichotokea.
 
Kwa hiyo tuseme unampenda NN kiasi hicho,!!!! nice one!!
 
Hofu yetu kubwa katika mapenzi ni kumpoteza umpendaye kwahiyo wivu hujengeka kwa kiasi flani dhidhi ya wale unaoona wanaweza kukuibia tunda lako.unachokihisi ni wivu ila si vibaya coz unaonesha unampenda mtu wako
 
...Ukimpenda, ukamwamini nawe ukajiamini...hutopatwa na wivu bali uchungu wa mapenzi



Wivu nm
1. hali au tabia ya mtu kusononeka au kukasirika muda mtu amuonapo mpenzi au rafiki yake ana uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine.
2. ngoa, kijicho, chonda, uhasidi, gere

Uchungu nm
hisia anazokuwa nazo mtu baada ya kufikwa na jambo la kuumiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…