...Hakuna kitu kinachoitwa limbwata nyie watu acheni kudanganyana. Kila siku tunawaambia kuwa nyie wanawake mlioolewa once mkishaingia kwenye ndoa mnajiamini kupita kiasi. Mnadhani mkishaolewa basi kazi imekwisha hamtaki kujishughulisha kuwajali waume zenu. Hivi vitabia vya kujifanya mnataka kuwa sawa na wanaume pia vinawapoteza, eti hutaki kuwa mnyenyekevu kwa mumeo kisa unajiona uko juu kwa kuwa umesoma na una kazi yenye mshahara mzuri so unaweza kushindana na mumeo. Mwanamke unatakiwa kuwa makini muda wote na kuhakikisha kuwa majukumu ya kumuhudumia mumeo yanabaki kuwa yako na si vinginevyo, wengine ndio wanahamishia usaidizi kwa wasichana wa kazi. Kuanzia kufua nguo ( tena mpaka chupi za mume), kupika chakula, kusafisha chumba, kutandika kitanda. Hizo nyumba ndogo zimegundua wanaume wenye ndoa wengi wao huwa frustrated na wake zao so wao wanapiga bao hapo hapo. Nyumba ndogo haoni tabu kumpa busu mwanaume, kumtengenezea chakula kitamu, wengine mpaka wanawaogesha wanaume kama watoto (utaacha kunogewa huko?), ukifika tu unapokewa kwa bashasha na pole kibao. Lazima mwanaume afarijike na ndipo ndoa zinapovurugika. Wito ni kuwa akina mama mlioko kwenye ndoa punguzeni kujiamini na ujeuri usiokuwa na maana. Hata wababa hakikisheni wake zenu mnawaweka karibu ingawa najua wengine mnakwazika na vijimambo vya wake zenu...........