Wakulaumiwa ni Mange Kimambi, na wale wote waliokaidi maagizo ya kutokuandamana siku ya uchaguzi. Maandalizi ya majeshi yetu hususani kwenye mazoezi na kauli zao za kutotaka watu wasiandamane siku ya uchaguzi, yalionesha wazi ni nini ambacho kingeenda kutokea endapo watu wangethubutu kuingiza pua zao barabarani kuandamana siku hiyo.
Sasa baadhi ya vijana ambao wengi wameshikiwa akili na Mange, akishirikiana na wakenya kadhaa walipuuza katazo la maandamano, na kujiona wana ubavu wa kuingia barabarani muda wote kuchoma vituo vyetu vya mabasi ya umma (mwendokasi), kuchoma magari ya watu, kuchoma maduka ya watu, yumba za watu, kuchoma vituo vya polisi, kuuwa polisi nk. I mean wakifikiri kwamba huo ndio ungekuwa mwisho wa serikali, hivyo hakuna atakaewafanya kitu.
Hawa watu wahakujua kwamba Mange alikuwa anawajaza upepo, huku yeye akitumia njia hiyo kupiga hela kwenye social media. Kumbuka kila alieingia kusoma, kusikiliza, na kuangalia post ya Mange Kimambi kwenye mitandao ya kijamii, iwe ni Instagram, YouTube nk hela ziliingia kwake kupitia views, subscribe nk. Wakati vijana walikuwa wanazidi kuingia barabarani kuumia, kuuwawa na wengine kukamatwa, yeye kwake ilikuwa furaha ya kuingiza mamilioni ya shilingi kupitia post zake mitandao.
Najua wapo ambao wameuwawa bila hatia, lakini je kama vijana wangesikiliza katazo la viongozi wa juu la kuwataka watu wasiandamane siku ya kupiga kura hayo yote yangetokea?
Waliambiwa wafanye maandamano yao siku nyingine ambayo sio ya uchaguzi, lkn wao wakakaidi, huku Mange akiwajaza upepo kuwa wanaweza. Sasa leo kati ya walioandamana, kuna walioacha watoto zao mayatima, huku watoto wa Mange wakiwa na wazazi wao wote wawili, kuna walioumia huku Mange akiwa mzima buheri.
Watu waliuwa polisi na kuchoma moto vituo, hivyo polisi na wao wakaona hii ishakuwa vita. Wakajihami na wao kuanza kuuwa kama wanavyouwawa. Vita haina macho na matokeo yake hata wasiohusika wakauwawa.
Waandamanaji wengine wakawa wanakimbilia vichochoroni, na kwenye makazi ya watu kujificha, hivyo polisi nao wakawa wanawarushia mabomu huko huko walipojificha, mwisho yale mabomu yakawa yanawaathiri watoto, wagonjwa na watu wengine ambao hawakuwepo kwenye maandamano. Kama waandamanaji wasingekuwa wanarushia polisi mawe, chupa na kukimbilia kujificha kwenye maeneo ya makazi ya watu basi madhara mengi yangeepukika.
Kila mchuma janga hula na nduguze. Mange kwa sasa hana cha kupoteza, ila aliowadanganya ndio waliopotea na kupotezwa. RIP kwa wote waliouwawa kwenye fujo zile.