Hii ni mbaya sana na imetuacha pabaya zaidi kama raia

Hivyo kwa akili yako na yenu hayo yana justify kuuwa,kuteka,kutesa nakadhalika,badala ya kujua vyanzo vya matatizo na kuvitafutia ufumbuzi?
Hili swali ungejiuliza wewe na Mange Kimambi kwamba kile kilichowafanya kuandamana siku ile ndio kili justify waandamanaji wachome nyumba za watu, wachome maduka ya watu, waunguze vituo na mabasi ya umma, waunguze vituo vya mafuta vya watu, wachome vituo na magari ya polisi, lkn zaidi wauwe mpaka polisi?

Mbona hili swala la hao waandamanaji kuuwa polisi haulizungumzi? Au unafikiri wao pekee ndio walistahili kuuwawa? Je lengo la kuchoma vitu hovyo NA kuuwa polisi lilikuwa nini? Je nyumba yenu ingekuwa jirani na vituo vya mafuta halaf ikashika moto kutoka kwenye kituo cha mafuta kilichounguzwa na kuuwa ndugu yako leo hii ungekuja hapa kutetea kilichofanywa?
 
Tatizo lenu baadhi yenu ni wanafiki. Unaandika jambo halaf unajificha kwenye kichaka cha siasa. Swala la kwenda kupiga kura au kutokupiga kura ni la kwako. Hapa tunazungumzia uhalisia wa kilichotokea.

1. Labda uniambie je waandamanaji walichoma vituo vya mafuta au hawakuchoma?

2. Waandamanaji hawakuchoma vituo vya mabasi ya mwendokasi au walichoma?

3. Waandamanaji hawakuchoma nyumba za watu na maduka au walichoma?

Waandamanaji hawakuchoma vituo vya polisi, magari na kuuwa polisi?

Je wale waliopata hasara za nyumba, magari nk ni nani atawafidia?

Na polisi waliouwawa ni nani atakaelipa uhai wao?

Hapo sijazungumzia hasara kubwa walizopata watu ambao gari zao ziliungulia kwenye vituo vya mafuta ambao baadhi hawakuwepo na wengine walikimbia kuokoa uhai wao na kuacha magari yao kwenye sheli za mafuta.

Lakini pia waandamanaji hao hao ndio waliokuwa wakitawanyika na kwenda kujificha mitaani, hivyo kupelekea polisi nao kuwapelekea moto huko huko wanapokimbilia kujificha. Hii inanikumbusha vita ya Hamas na Israel ambapo Hamas walikuwa wanafanya mashambulizi na kukimbilia kujificha kwa raia. Israel nayo kwa kutokujua nani raia na nani Hamas ikawa inafyeka yoyote wanaemkuta kwenye eneo husika.

Hivyo wale waandamanaji wasingeharibu mali, miundombinu, au wasingeuwa polisi na kukimbilia kujificha walipo raia wengine hayo yote yasingetokea.

Nina uhakika kama waandamanaji wangeachwa waendelee kufanya walichofanya nina uhakika leo hii maeneo mengi ya bongo nyumba na maduka vingebaki majivu na watu waliokuwa ndani ya nyumba hizo pengine wangekuwa wameuwawa wengi.
 
First let me correct you, kupiga kura sio kuchumbia to call it personal, its a civic duty!
Pili, kuna mahali nimesifu mauaji ya polisi? Mauaji ni mauaji tu, kwa vyovyote vile hayakubaliki!
Ninakushangaa na nitaendelea kukushangaa kuwa unaona mauaji ya polisi ni jambo baya lakini mauaji ya waandamanaji ni sawa! Kwahilo niko tayari kuitwa mnafiki!
Wewe ungekuwa sio mnafiki, kwenye hili ungekubaliana na mimi kuwa vyombo vya dola kwa upande mmoja na waandamaji kwa upande mwingine wote hawawezi kukwepa lawama kwa madhila haya.
Ni vyema tujiulize tumefikaje hapo, tufanye tathmini ya kina, wahalifu wafikishwe mahakamani na tujipange haya yasitokee tena badala ya kukaa na kusubiri maandamano mengine yatokee tena.
Kama tungejenga utamaduni wa kusikilizana, kuchukuliana na kuvumiliana pengine tungeyaepuka haya.
 
Nilikuwa nishaanza ku move on kwenye hili ili andiko linanirudisha tena aisee maumivu ni makubwa mnoo
 
Mkuu kumbe wewe ni muungwana sana, hivyo acha na mimi nikujibu kiungwana.

Inawezekana ukawa haujui kweli kwamba haya mambo ya machafuko yalitaka kuepushwa na serikali, ila kwa upande wa waandamanaji wao walikuwa na agenda yao ya siri hivyo walipinga kile walichoambiwa.

Hawa watu waliambiwa wasiandamane siku ya kupiga kura kwani ingeweza kuleta mtafaruku mkubwa sana baina ya wapiga kura na wasiopiga kura. Hivyo wakatakiwa wapange siku nyingine nje ya siku ile ya kupiga kura. Kumbuka tarehe ya uchaguzi ilikuwa imeshapangwa muda mrefu kabla hata ya kupangwa maandamano hivyo waandamanaji wao ndio walitakiwa wachague siku nyingine na sio ile ya uchaguzi.

Mbali na kushauri na vyombo husika, pia kuna mwana Chadema fulan anaitwa anti Lulu akiingia kwenye YouTube na vyombo vingine vya habari utampata. Na yeye aliwahi kushauri wenzake kwamba wabadilishe siku ya maandamano na sio siku ile ya kupiga kura kwani siku hiyo ipo kikatiba, hivyo iheshimiwe.

Sasa kwa upande wa wanaopanga maandamano ambao asilimia kubwa wapo nje ya Tz na wengine wapo lkn hawakutoka kuandamana wakapinga swala hilo wakidhani labda maandamano yao yataweza kabisa kuharibu ratiba nzima ya uchaguzi hivyo lengo lao la kuharibu uchaguzi litakuwa limetimia. Wakasahau kwamba serikali huwa haishurutishwi na genge la watu kufanya jambo haswa linapokuwa lipo kikatiba kama hilo la siku ya uchaguzi.
Polisi walijaribu kuwambia waandamanaji warudi majumbani kwao kwa vile siku hiyo ni ya uchaguzi kikatiba na hawana vibali vya kuandamana, lkn wao wakakaidi na mbaya zaidi wakaanza kuvamia vitu na kuanza kuiba, kuchoma NA kuharibu. Polisi kwa vile kazi yake ni kulinda mali za raia wakaanza kutumia mabomu kuwatawanya, ila badala ya kutawanyika ikawa kama vile moto unaongezwa mafuta.
Ila hali iliyopo sasa wananchi na police hawaaminiani, wananchi hawawaoni police kama rafiki zao, ndio maana Confrontation nadhani ilikuwa kubwa.
Mkuu tukubali tukatae Ila ukweli utabaki pale pale kwamba waandamanaji walikuwa na malengo yao mengine nje na yale unayoyajua wewe. Ndomaana walichoma vituo vya mafuta, walichoma magari, walichoma maduka, walichoma nyumba, walichoma vituo vya polisi na mbaya zaidi waliuwa mpaka polisi

Hivi waandamanaji gani wanasema tukamtembelee fulan wanakwenda na kuunguza duka lake, nyumba yake au gari lake? Je hayo ni maandamano kweli? Mbona ni kama vile walikuwa wanataka wao ndio watawale nchi? Muandamanaji anapata wapi nguvu na sheria ya kwenda kuchoma kitu cha mtu au kuiba?

Bila shaka siku ile kuna watu walikuwa wanataka serikali ianguke. Jambo ambalo ni ngumu sana. Hii ya kutopambana na jeshi ni kwa sababu yule mwanajeshi uchwara anaeitwa tesha aliwahadaa kwamba jeshi lipo katika maandalizi ya kuchukua nchi ndomaana wapo mitaani kuwalinda waandamanaji 🤣🤣🤣🤣

Hata mimi ningeshangaa serikali ianguke kwa sababu ya mipango ya Mange Kimambi na genge lake aisee.
 
Nashukuru kwa kunielimisha, mwisho tumshukuru Mungu tumevuka salama.
 
Mange aliwadanganya sana vijana wa Jay Z, eti aliwaambia jeshi litawalinda, halafu hakuwapa plan yoyote , wala hawakua na kiongozi, wala hawakua sehemu ya kupeleka malalamiko yao, maandamano yoyote huwa yana sehemu ya kuanzia na kuishia pamoja na hoja za kuwasilisha, lakini vijana wa Jayz hawakujua nn cha kufanya matokeo yake wakaanza kuharibu miundombinu na kuchoma mali za raia.

Lakini pia Mangereza hakuwatayarisha kisaikolojia na athari hasi za maandamano, walijua tu wataingia barabarani halafu watarudi makwao kula ubwabwa na samia atajiuzulu, big mistake
 
Nyie jamaa munatilisha huruma kwa kitu ambacho it was bound to happen, sasa munapokuja na reaction kama vile munashangaa yalioyotokea hapo ndipo huwa nakushangaeni.
Nyinyi wenyewe kabla ya hayo maandmano mulikuwa munajinadi munajiandaa kufa au mulikua munatania? CCM ni masheteni mulitakiwa muelewe hilo na linaokuja suala la kulinda madaraka yao wanakuwa zaidi ya shetani.
Inasikitisha sana
 
Kabisa mkuu, nimegundua hawa akili zao hazipo sawa sawa na utimamu wao upo questionable.
Hii ishu watu wahazungumzii Nini kiini au chanzo Cha hili Tatizo kutokea.
Wengi wanaongelea kuhusu madhara ya mali za watu.

Hawaongelei chanzo Cha tatizo, (source ya tatizo) na vifo vya watu.
Watu wanarukaruka tu. Utafikili kama ni ujinga hivi.
 
Tunasubiri GUN violence kati ya police na jwtz pamoja na kikundi.
 
Kama wewe ni mtaalam wa kusoma body language za watu utagundua vizuri kuwa Mange ni muongo muongo anaeokoteza maneno ya kuwahadaa wajinga kwa ajili yake NA wenzake. Yani ni mtu ambae anapambania tumbo lake na watoto wake. Hawa watoto wa masikini wanaoingia barabarani kufa, kuumizwa na kukamatwa kwa ajili ya mipango yake hawajali wala kuwathamini.

Leo hii waliohadaiwa kuandamana wameuwawa yeye bado yupo hai anabadilisha mitindo ya nywele tu na kwenda shopping kutumia hela alizoingiza katika kipindi hiki kupitia wale waliosoma, waliosikiliza na kuangalia post zake huko Twitter, Instagram, YouTube, FB nk.

Watoto wake wanasoma shule za gharama, huku watoto wa waandamanaji wakibaki mayatima kwa ajili ya upumbavu na ujinga wa wazazi wao. Ama kweli kila mchuma janga hula na wa kwao.
 
CCM kadili miaka inavyoenda ndivyo kinazidi kuwa na kiburi.
Na mostly ya watu wake Wana low thinking capacity,
Ni hatari sana
 
Pia anatembelea G wagon alioipata kwa kazi ya umbea na kuuza video za uchi za watanzania, sitasahau siku alivokianika kitumbua cha Irene Uwoya
 
Hii ishu watu wahazungumzii Nini kiini au chanzo Cha hili Tatizo kutokea.
Wengi wanaongelea kuhusu madhara ya mali za watu.

Hawaongelei chanzo Cha tatizo, (source ya tatizo) na vifo vya watu.
Watu wanarukaruka tu. Utafikili kama ni ujinga hivi.
Hawa ni wale ambao muda wote before 29 October day walikuwa wanajitoa ufahamu na kushiriki kikamilifu katika siasa as if hawaoni maovu na ukiukwaji wa sheria unaoendelea. Saa hii macho yanawatoka kwasababu wanastaajabu kuona wale waliowashangilia ndio wanafanya uharamu kwa raia na sasa wanashindwa walaumu wanabakia kunyooshea vidole kwa watu wasiohusika.
 
Mara ya kwanza walikuwa wanasema mkiandamana mtakiona Cha moto ,
Sasa wanashangaa watu wao waliowatetea ndo wamefanya uhalifu wa mauaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…