hii ni mimba au

hii ni mimba au

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,164
Reaction score
1,293
Salama humu ndani?
Jamani naombeni mnipe uzoefu nyie ambao mmeshakua na watoto na mna uzoefu hata kupitia vitabu tofauti.
Ovulation day ya wife wangu ilikua ni tar 12/9 na ndo kwake ilikua siku ya 14 na kwa kawaida ya mzunguko wake ilitakiwa awe ameshaingia m.p lakini mpaka sasa tar 23/9 bado hajaingia.
Kinachonifanya niulize ni namna anavyojisikia, yani dalili zote za bleed anazipata nyakati za asubuhi kiuno kinamuuma na matiti kuna mda anasema yanauma lakini ikifika mchana zinapotea anakua ok ila anapata uchovu ikifika jioni.
Mpaka sasa yupo fiti hakuna bleed japo dalili anaziona zinakuja na kupotea hebu nambieni hii ni hali ya kawaida au vipi.
Je kitaalam mimba inaanza kuonekana siku ya ngapi baada ya ovulation manake tumenunua kipimo jana kimesoma negative hebu nitoeni hofu wana jamii hapa. Kwa swali lolote niulizeni jaman labda sijsjieleza vizuri.
 
Ngoja nitarudi maana naona kama maelezo yako yanajichanganya
 
Ngoja nitarudi maana naona kama maelezo yako yanajichanganya

wapi nimejichanganya mkuu nirekebishe fasta na ndo mana nikasema kama kuna mahali sijaeleweka mnambie niweke sawa
 
Salama humu ndani?
Jamani naombeni mnipe uzoefu nyie ambao mmeshakua na watoto na mna uzoefu hata kupitia vitabu tofauti.
Ovulation day ya wife wangu ilikua ni tar 12/9 na ndo kwake ilikua siku ya 14 na kwa kawaida ya mzunguko wake ilitakiwa awe ameshaingia m.p lakini mpaka sasa tar 23/9 bado hajaingia.
Kinachonifanya niulize ni namna anavyojisikia, yani dalili zote za bleed anazipata nyakati za asubuhi kiuno kinamuuma na matiti kuna mda anasema yanauma lakini ikifika mchana zinapotea anakua ok ila anapata uchovu ikifika jioni.
Mpaka sasa yupo fiti hakuna bleed japo dalili anaziona zinakuja na kupotea hebu nambieni hii ni hali ya kawaida au vipi.
Je kitaalam mimba inaanza kuonekana siku ya ngapi baada ya ovulation manake tumenunua kipimo jana kimesoma negative hebu nitoeni hofu wana jamii hapa. Kwa swali lolote niulizeni jaman labda sijsjieleza vizuri.

huyo mkeo au kabinti ka std iv?
 
Ovulation day ya wife wangu ilikua ni tar 12/9 na ndo kwake ilikua siku ya 14

Unawezaje kufahamu exact date ya ovulation ya huyo mwanamama?

Anyway lets assume yo right...

na kwa kawaida ya mzunguko wake ilitakiwa awe ameshaingia m.p

Kama ambavyo umeeleza hapo juu kuhusu habari za ovulation na tarehe hiyo...

Ni dhahiri kuwa jumla ya siku zote za mzunguko za mwanamama huyo ni 28 (plus or minus)...

Na kama ukihesabu kuwa kwa kudhania kuwa tar 12/9 ndio siku ya 14, basi siku ya 28 itaangukia tar 26....

Kwa fact hiyo kuna uwezekano next MP ikaanza pengine tar 28 yenyewe, tar 29 etc...

Hivyo kutokuingia kwake MP kwa sasa kwangu naona ni sahihi kwa kadiri ya maelezo uliyotoa
 
Ngoja nitarudi maana naona kama maelezo yako yanajichanganya

mzunguko wake ni mfupi kati ya siku 25 au 26 na ni mara chache sana kutokea changes katika hiyo time table yake na sisi tulisex siku ya 14 baada ya siku ya kwanza ya mp yake ambayo kitaalam ndo siku exactly ya ovulation so kwa mzunguko huu mfupi nafkiri alitakiwa awe tayari ameingia au? Anyway ishu ni mimba huanza kuonekana baada ya muda gani
 
Kuumwa kiuno,
Kuumwa matiti,
Kuchoka...
BHAS HIYO NI MIMBA 49%
 
mzunguko wake ni mfupi kati ya siku 25 au 26 na ni mara chache sana kutokea changes katika hiyo time table yake na sisi tulisex siku ya 14 baada ya siku ya kwanza ya mp yake ambayo kitaalam ndo siku exactly ya ovulation

Mkuu watu wengi huwa confused na siku haswa ya ovulation na kwa wasio tayari kupata habari za ujauzito wamejikuta wakinaswa katika shida hii...

Siku ya 14 si lazima iwe ndio siku ya ovulation kwa kila mwanamke isipokuwa it's a calculated value kwa wale wenye mzunguko wa siku 28 pekee...(inaaminika hivyo kwa watu wa siku 28 pekee)...

Hesabu inayotumika si kugawanya siku 28 mara mbili, isipokuwa hesabu sahihi ni kuchukua idadi kamili ya mzunguko wa mwanamke halafu unatoa kwa 14 (hili wengi hawalijui)...

Sasa kama mkeo siku zake za mzunguko ni 25 au 26, hesabu yake ni 25 kutoa 14 which is 11 au 26 kutoa 14 which is 12...

11 au 12 ndio siku inayotarajiwa kuwa ni ovulation kwa mwanamke huyo na hesabu yake inaanza tokea siku ya kwanza alipoona MP...

so kwa mzunguko huu mfupi nafkiri alitakiwa awe tayari ameingia au?

Kimahesabu kama ulivyotueleza MP inabidi aanze kuiona kesho au keshokutwa...mara nyingi dalili za ujauzito na MP huwa hazipishani sana hivyo wakati mwingine ni ngumu kutambua.

Anyway ishu ni mimba huanza kuonekana baada ya muda gani

Kawaida huwa ni wiki moja tangu mwanamke alipotarajia kuona MP yake...
 
shukrani sana wakuu ngoja tuzidi kuskilizia tuone itakavyokua manake wengine wananambia kuwa siku ya 14 sio siku ya ovulation so nalazimika kuwa mpole kama itakua negative itanilazm kujipanga tena next month kwa umakini zaidi. Nahitaji sana sana mtoto
 
Back
Top Bottom