- Source #1
- View Source #1
Wakuu wa JamiiCheck naomba msaada wa kuthibitisha picha hii maana imesambaa sana mtandaoni, nashindwa kutofautisha kama ni halisi au AI generated.
- Tunachokijua
- Sadio Mané ni mchezaji wa mpira wa miguu ambaye ni nahodha na mfungaji bora wa kihistoria wa timu ya taifa ya Senegal. Alijiunga na klabu ya Saudi Pro League, Al Nassr, akifuata nyayo za Cristiano Ronaldo, baada ya kutumikia msimu wa 2022-23 katika klabu ya Ujerumani, Bayern Munich akitokea Liverpool FC.
Timu yake ya Zamani Liverpool inamuelezea Sadio kama mshambuliaji aliyetumikia timu hiyo kwa misimu sita yenye ubora wa hali ya juu na alikuwa mmoja wa wachezaji wa muhimu waliosaidia klabu hiyo kushinda mataji makubwa kadhaa chini ya uongozi wa Jürgen Klopp.
Sadio alioa katika sherehe ya faragha na mpenzi wake wa miaka 19, Aisha Tamba, siku chache tu kabla ya kuondoka kuelekea Ivory Coast kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 na Senegal,
Madai
Ipo picha inayosambaa mtandaoni ikimuonesha Mané na anayedaiwa kuwa mke wake wakiwa na watoto wawili wanoonekana kuwa ni mapacha, ambapo imetumika kuwapongeza kwa kujaaliwa kupata watoto hao.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa picha si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde kwani hakuna picha rasmi kama hiyo iliyotolewa na familia ya Mane.
Vivile anayedaiwa kuwa mke wa Sadio katika picha hiyo si kweli kuwa ni mkewe bali ni Eva Touré, aliyefanya mahojiano na Sadio Mané ambapo mavazi waliyovalia yanafanana na yale waliyovaa kwenye picha.
Aidha tovuti ya BuzzSenegal ilichapisha picha ya mtangazaji huyo wakiwa na Sadio pasipo watoto wachanga na kuweka kichwa cha habari 'Sadio Mané kwenye kipindi cha Confidence? Taarifa mpya ya Eva Loyalty kupitia Instagram'
JamiiCheck ikaenda mbali zaidi ili kuthibitisha endapo picha hiyo ilichapishwa na mtangazaji huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo ilibaini kuwa ni kwe kama ilivyoelezwa na Tovuti BuzzSenegal. Tazama picha halisi hapa.
Aidha hakuna chanzo cha kuaminika kilichoripoti kwamba Mané na na mkewe Tamba wana watoto mapacha, isipokuwa wawili hao wamejaaliwa kupata mtoto mmoja.
Machi 13, 2025 timu yake ya Al Nassr kupitia ukurasa wa X ilimpongeza Sadio kwa kupata mtoto wake wa kwanza "Tunampongeza nyota wetu Sadio Mané kwa ujio wa mtoto wake wa kwanza. Mwenyezi Mungu amjalie mema, na Mwenyezi Mungu amfanye kuwa miongoni mwa wateule wake wa haki." - Iliandika timu hiyo katika ukurasa wake wa X.
Na baada ya kufunga bao la ushindi katika mechi dhidi ya Al-Kholood timu yake iliposhinda bao 3 kwa 1 mchezaji huyo alishangilia kwa njia ya kipekee na kuongeza kuwa ni sehemu ya kumkaribisha mtoto wake wa kwanza duniani.
Picha halisi