Hii ni sawa?

TEK

Senior Member
Joined
Jul 13, 2015
Posts
184
Reaction score
35
Nilipomaliza kidato cha sita nilipata kazi ya kufundisha katika shule moja ya binafsi huku mkoani kwangu.Baada ya mwaka mmoja niliomba kwenda masomoni.

Baada ya kumaliza masomo nilirudi tena pale nilipokuwa, nikafanya kazi kwa muda hadi nilipopata ajira serikalini, baada ya kutoka kwenda serikalini nilipwlekwa polisi baadae mahakamani na mahakama ikaamuru nilipe milioni kama 2 kasoro hivi.

OMBI KWENU: Mimi naomba kwa wenye ujuzi wa haya mambo yanayohusiana na kazi pamoja na haki za waajiri na waajiriwa wanisaidie wapi nilikosea?

NB: Kuna mambo hapo nimeyashorten ilikuifupisha tu hii thread.
 
umeifupisha sana,kata haieleweki.kwa nini ulipelekwa mahakamani?
 
Walinipeleka mahakamani kuwa mimi nadaiwa nao. Labda niseme hivi kunawakati nilipokuwa nasoma chuo walikuwa wananipa laki 2 kwa mwezi. Ilamimi nilikuwa naenda kufanya kazi kwao kila likizo ya chuo. Wao maelezo walopeleka mahakamani ni kuwanatakiwa nilipe hela yao niliyolipwa wakati niko chuo
 
je mulikuwa na mkataba kuwa baada ya chuo ufanye kazi miaka mingapi ktk shule yao
 
sijui aina za mikataba ilasikuandika mkataba
 
Kwa kifupi ndugu kama hakukuwa na mkataba wowote wa maandishi juu ya makubaliano ya kazi basi hakuna kosa. vile vile kama mlikubaliana kwa maneno na hakuna shahidi pindi mnakubalina basi you are safe..... LAKINI swali litakuja kwanini ulikua unapokea monthly salary kipindi ambacho hukuwa hata unawafanyia kazi kwa kifupi they were investing on you and they definitely need their return.

Mimi si mtaalamu wa sheria lakini hayo ni mawazo yangu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…