Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Kumekuwa na matumizi mabaya ya kukera ya simu.

1. Mtu anakupigia simu hujapokea anaendelea kupiga tena na tena. Ukija mpigia baadaye unamuuliza shida nini anakwambia alikuwa anakusalimia tu. Ukiona umepiga simu mara moja mtu hajapokea acha usumbufu. Tulia akiwa Ok atakupigia.

2. Mtu hakudai wala nini anakupigia hupokei anaenda tafuta namba mpya kuendelea kukupigia. Hana jambo la maana anataka mpige stories. Hii tabia ya kukera.

3. Saa nne usiku mtu anakupigia simu mpige stories. Why? Usiku ni muda wa kupumzika wadau heshimu mapumziko ya mwenzio.

4. Mtu anakupigia unamsalimia anakujibu. Then anakwambia "Niambie" inashangaza sana.wewe umenipigia then unataka mimi ndo nikwambie. Nikwambie nini? Ingekuwa na kukwambia ningekupigia.

5. Mtu anakupigia simu kwa namba ngeni unamuuliza nani mwenzangu. Anakwambia ina maana sauti yangu huifahamu/umeisahau? Huu ni upumbavu, mimi sina jukumu la kukariri sauti yako.

6. Kuna wale toka wafahamu whatsapp video call imekuwa nongwa. Ikitokea tu kakuona online haraka video call. Huu si ustaarabu. Watu wanataka privacy. Omba kwanza kama its possible kupiga upate kibali.

7. Tabia ya kupiga simu halafu unalalamika. Mbona umekaa muda mrefu hujanipigia simu ni upuuzi kama sijakupigia simu ni kwamba sikuwa na cha kukwambia. Kama unacho piga ongea siyo kuambiana nipe story...

Tutumie simu ipasavyo kama huna cha kuongea na mtu tulia tu. Au salimia kifupi tu basi. Watu tuna mambo mengi kichwani siyo kuleteana habari sizizo na kichwa wala miguu.
 
Kuna ile:
My wangu: Vipi baby wafanya nini?
Me: Niko kitandani nataka kulala bb
My wangu: Ahaah sawa mambo mengine vipi bby?
Me: Yako poa vipi huko?
My wangu: Sawa baby mic u mwaaah[emoji849]
Me: Me too luv
My wangu: Asante bby mambo mengine vipi?
Me : Yako poa mpz
My wangu: Mambo yanaendaje lakini?
Me: Tuko poa kwakeli
My wangu: Kwa hiyo ndo unalala bby?
Me: Ndio. Si nimekwambia niko kitandani!.
My wangu: Sawa baby mambo yanaenda vizuri lakini? Unalala zako kwa raha zako

Unaweza kumpigia simu mama, baba yake ukawatukana kwa kuzaa kilaza.
Ukampiga block ya maisha.
 
Na mimi nina langu.
Unakuta mtu mnafanya kazi pamoja, kuna taarifa muhimu inatakiwa aipate labda kusaini doc fulani ya muhimu. Unampigia simu, unampigia simu hapokei na wala hakuna call back, unaamua kutuma msg nayo kimya hajibu. Unajisemea tu shauri yake! Ishu imetiki na yeye kakosa kwa sababu hakuna sahihi yake, anaanza kukulaumu eti mbona hukuniambia! Una roho mbaya.

Unamwambia lete simu yako nikuoneshe calls zangu na sms nilizotuma. Masikini unakuta kumbe sms hakusoma, hata missed call alizicancel tu na kuendelea na simu mpya tu.

Hii tabia wanayo ndugu zetu wanaoweka simu kwenye pochi, ingawa na wanaume baadhi wanayo hii tabia. Yaani hata ukiwa na shida naye nyumbani, mpaka upige simu ya jirani ndio utaongea naye.

POVU SIO RUKSA.
 
Kuna ile:
My wangu: Vipi baby wafanya nini?
Me: Niko kitandani nataka kulala bb
My wangu: Ahaah sawa mambo mengine vipi bby?
Me: Yako poa vipi huko?
My wangu: Sawa baby mic u mwaaah[emoji849]
Me: Me too luv
My wangu: Asante bby mambo mengine vipi?
Me : Yako poa mpz
My wangu: Mambo yanaendaje lakini?
Me: Tuko poa kwakeli
My wangu: Kwa hiyo ndo unalala bby?
Me: Ndio. Si nimekwambia niko kitandani!.
My wangu: Sawa baby mambo yanaenda vizuri lakini? Unalala zako kwa raha zako

Unaweza kumpigia simu mama, baba yake ukawatukana kwa kuzaa kilaza.
Ukampiga block ya maisha.
😂😂
Looh ha ha ha ha kweli "kilaza"...
Maskini maneno yote hayo hwenda ikawa yuko h..orn.....y na ameshikika haswa...sasa anahisi akiendelea kuuliza "kizwazwa" inaweza kutokea maajabu "my wake" akapeperushiwa na upepo kutoka huko aliko na awe nae kitandani muda huo😁😁..
 
Back
Top Bottom