Kumekuwa na matumizi mabaya ya kukera ya simu.
1. Mtu anakupigia simu hujapokea anaendelea kupiga tena na tena. Ukija mpigia baadaye unamuuliza shida nini anakwambia alikuwa anakusalimia tu. Ukiona umepiga simu mara moja mtu hajapokea acha usumbufu. Tulia akiwa Ok atakupigia.
2. Mtu hakudai wala nini anakupigia hupokei anaenda tafuta namba mpya kuendelea kukupigia. Hana jambo la maana anataka mpige stories. Hii tabia ya kukera.
3. Saa nne usiku mtu anakupigia simu mpige stories. Why? Usiku ni muda wa kupumzika wadau heshimu mapumziko ya mwenzio.
4. Mtu anakupigia unamsalimia anakujibu. Then anakwambia "Niambie" inashangaza sana.wewe umenipigia then unataka mimi ndo nikwambie. Nikwambie nini? Ingekuwa na kukwambia ningekupigia.
5. Mtu anakupigia simu kwa namba ngeni unamuuliza nani mwenzangu. Anakwambia ina maana sauti yangu huhifahamu/umeisahau? Huu ni upumbavu, mi sina jukumu la kukariri sauti yako.
Tutumie simu ipasavyo kama huna cha kuongea na mtu tulia tu. Au salimia kifupi tu basi. Watu tuna mambo mengi kichwani siyo kuleteana habari sizizo na kichwa wala miguu.