Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

Hapana. Nliambiwa nikaenda mwangalia. Yule hayupo smart kama mimi.mwandiko wake mbaya,una makosa.hana akili za kumwagika.pia si handsome so hata hapati mademu wakali.ingawa kachukua avatar yangu lakin mademu wakienda onana naye live wanamkimbia. Pia nasikia anauzia watu sijui vitabu gani. Mimi Gudume siwezi weka namba yangu kwenye mtandao kwa any business

Maana mbwembwe na machachari yake ni kama yako tu...


Cc: mahondaw
 
Hizo ni Tabia za wanafunzi na washamba washamba.
 
Hiyo namba moja unaniudhi sana, unakuta mtu anapiga simu hupokei anaendelea kupiga tuuuuuuu...hata mara ishirini! Ukipiga simu mara moja au mbili na haipokelewi, chili..uliyempigia ataiona, atakupigia au andika text message..damn
huyu ni jamaa yangu anatwanga simu hata mara 10+ badae analaumu kwamba nilikuwa nimeweka kwenye mtetemo ndo maana sisikii simu kumbe nakuwa na mambo mengine.
 
Anakuwa na jambo gani nyeti hivyo?

huyu ni jamaa yangu anatwanga simu hata mara 10+ badae analaumu kwamba nilikuwa nimeweka kwenye mtetemo ndo maana sisikii simu kumbe nakuwa na mambo mengine.
 
Kuna ile unamtafuta mdada anakuuliza namba yangu umeitoa wapi, halafu ukimpotezea analalama hana bahati. Karne ya namba yangu umeitolea wapi ishapitwa tayari. Ukipigiwa tulia kama vocal hazipandi unachomoa life linasonga.
 
Zamani wakati sim ikiwa ni huduma adim, kitendo cha kupokea simu au kupiga kilikuwa ni kitendo maalum sana na kwa sababu kubwa za msingi tu. Zilipoingia simu za kiganjani zilikuta watu wana hamu ya kupiga simu sana. Baadhi ya watu wamechelewa sana kumiliki hizi simu za viganjani na hamu zao za kupiga simu bado zipo juu sana.
Hivyo mkuu wasikukwaze sana ,ni swala la muda watakuja kuchoka wenyewe.
 
Basi hayupo smart. Mi kuna mmoja nlimwambia akagundua amenikwaza. Alinipigia sana kwa simu yake akaona sipokei.akawa anatumia nyingine siifahamu.sikupokea nlihisi tu ni yeye.baadaye nikampigia kwnza kwa namba yake.then nlipomaliza nikampigia kwa ile nyingine nako akapokea. Nikamuuliza nani mwenzangu akajibu flani.nikamwambia sasa uliona sipokei kwenye namba ile ukaamua kupiga kwa hii kwani unanidai?ukiona mtu hapokei simu jua yupo busy au una dharura gani?akakosa majibu nikakata simu.


basi kuna unyeti wowote basi tu kero na ujinga wake na huwa sipokei makusudi tu nashangaa ajastukia
 
Kumekuwa na matumizi mabaya ya kukera ya simu.

1. Mtu anakupigia simu hujapokea anaendelea kupiga tena na tena. Ukija mpigia baadaye unamuuliza shida nini anakwambia alikuwa anakusalimia tu. Ukiona umepiga simu mara moja mtu hajapokea acha usumbufu. Tulia akiwa Ok atakupigia.

2. Mtu hakudai wala nini anakupigia hupokei anaenda tafuta namba mpya kuendelea kukupigia. Hana jambo la maana anataka mpige stories. Hii tabia ya kukera.

3. Saa nne usiku mtu anakupigia simu mpige stories. Why? Usiku ni muda wa kupumzika wadau heshimu mapumziko ya mwenzio.

4. Mtu anakupigia unamsalimia anakujibu. Then anakwambia "Niambie" inashangaza sana.wewe umenipigia then unataka mimi ndo nikwambie. Nikwambie nini? Ingekuwa na kukwambia ningekupigia.

5. Mtu anakupigia simu kwa namba ngeni unamuuliza nani mwenzangu. Anakwambia ina maana sauti yangu huhifahamu/umeisahau? Huu ni upumbavu, mi sina jukumu la kukariri sauti yako.

6. Kuna wale toka wafahamu whatsapp video call imekuwa nongwa.ikitokea tu kakuona online haraka video call. Huu si ustaarabu. Watu wanataka privacy. Omba kwanza kama its possible kupiga upate kibali.

7. Tabia ya kupiga simu halafu unalalamika. Mbona umekaa muda mrefu hujanipigia simu.ni upuuzi.kama sijakupigia simu ni kwamba sikuwa na cha kukwambia. Kama unacho piga ongea.siyo kuambiana nipe story...

Tutumie simu ipasavyo kama huna cha kuongea na mtu tulia tu. Au salimia kifupi tu basi. Watu tuna mambo mengi kichwani siyo kuleteana habari sizizo na kichwa wala miguu.
Seconded
 
Back
Top Bottom