Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

Tabia inayonikera ni mtu wa pembeni yako kapigiwa simu, ghafla anaropoka nipo na fulani hapa chukua umsalimie! 😏😏🙄
 
Mtu anakulalamikia kakutumia msg humjibu,unamuuliza umenitumia lini msg? anajibu jana whatsapp

unamuuliza,hivi aliekwambia nipo whatsapp nani? anakujibu "nimekuona online siku ile mbona"

wananiboaga hawa raia acha tu,yani kuna watu msg za kawaida hatumi hata kwa bahati mbaya ila subiri

akuone upo ONLINE whatsapp lazima tu utamuona huyooo,ki ukweli najibugi tu ili wasinione nadharau ila sipendi...
 
🤔🤔 Nimekuja kujua kumbe wengi tunakerwa sana na hizi tabia tajwa apo juu hasa,,anapiga af anakuambia niambie,,unamuuliza we nan anasema kwani hunijui ,, mara mbna hunitafuti au umenisahau,, nataman ujumbe uwafikie ipasavyo maana ata kuwaambia direct inakuwa ni kazi




Kuna hii ingine apa,,


Unakuta mtu mnakaa nae kitaa kimoja ila kila siku akikutafta anaishia kukuambia mbona huonekani ase,,mara mbna hujagi huku kwetu(n:b ye kwetu hajagi Ila anapajua)
Mara mbona umejifungia hivyo

Ni vyema basi kama unashida sana ya sis kuonana uwe unakuja basi ninapoishi..,sio kulalamika kila siku
 
shida inayonikera ni pale ninapopiga simu halafu hata sijamaliza ongea unakata miache alokupigia ndiye akata
 
Kumekuwa na matumizi mabaya ya kukera ya simu.

1. Mtu anakupigia simu hujapokea anaendelea kupiga tena na tena. Ukija mpigia baadaye unamuuliza shida nini anakwambia alikuwa anakusalimia tu. Ukiona umepiga simu mara moja mtu hajapokea acha usumbufu. Tulia akiwa Ok atakupigia.

2. Mtu hakudai wala nini anakupigia hupokei anaenda tafuta namba mpya kuendelea kukupigia. Hana jambo la maana anataka mpige stories. Hii tabia ya kukera.

3. Saa nne usiku mtu anakupigia simu mpige stories. Why? Usiku ni muda wa kupumzika wadau heshimu mapumziko ya mwenzio.

4. Mtu anakupigia unamsalimia anakujibu. Then anakwambia "Niambie" inashangaza sana.wewe umenipigia then unataka mimi ndo nikwambie. Nikwambie nini? Ingekuwa na kukwambia ningekupigia.

5. Mtu anakupigia simu kwa namba ngeni unamuuliza nani mwenzangu. Anakwambia ina maana sauti yangu huhifahamu/umeisahau? Huu ni upumbavu, mi sina jukumu la kukariri sauti yako.

6. Kuna wale toka wafahamu whatsapp video call imekuwa nongwa.ikitokea tu kakuona online haraka video call. Huu si ustaarabu. Watu wanataka privacy. Omba kwanza kama its possible kupiga upate kibali.

7. Tabia ya kupiga simu halafu unalalamika. Mbona umekaa muda mrefu hujanipigia simu.ni upuuzi.kama sijakupigia simu ni kwamba sikuwa na cha kukwambia. Kama unacho piga ongea.siyo kuambiana nipe story...

Tutumie simu ipasavyo kama huna cha kuongea na mtu tulia tu. Au salimia kifupi tu basi. Watu tuna mambo mengi kichwani siyo kuleteana habari sizizo na kichwa wala miguu.
Well spoken Gudume katika ubora wako.
 
Kuna ile:
My wangu: Vipi baby wafanya nini?
Me: Niko kitandani nataka kulala bb
My wangu: Ahaah sawa mambo mengine vipi bby?
Me: Yako poa vipi huko?
My wangu: Sawa baby mic u mwaaah[emoji849]
Me: Me too luv
My wangu: Asante bby mambo mengine vipi?
Me : Yako poa mpz
My wangu: Mambo yanaendaje lakini?
Me: Tuko poa kwakeli
My wangu: Kwa hiyo ndo unalala bby?
Me: Ndio. Si nimekwambia niko kitandani!.
My wangu: Sawa baby mambo yanaenda vizuri lakini? Unalala zako kwa raha zako

Unaweza kumpigia simu mama, baba yake ukawatukana kwa kuzaa kilaza.
Ukampiga block ya maisha.
Yooote yaliyopita ni chamtoto, hii ndo kiboko kweli. Umenifanya nicheke sana mkuu
 
Hii "niambie" "leta story" "kuna mapya gani huko" boring sana
Gudume naye anasema tu, hivi mchuchu km Numbisa anipigie anambie lete story? nita boreka kweli labda usiwe mwanaume!

yaani ndo kwanza unamtumia Salio la kutosha. utasikia.. heeh!! nilikuwa nakutafuta Baby nkutumie ya Lunch! ..baby yaani naona damu zetu zinalandana kweli tumechaguana, nikikuwaza na wewe unaniwaaza raha sana sijawahi ona, !!! nikutayarishe nini leo baby???.. Amalula ya Blue.
 
Mtu anakupigia kwa namba ngeni, unapokea 'haloo' nae anaitika 'haloo' eboo si uongee
Mwingine anakupigia simu unapokea, unamuuliza we nani? Anagundua amekosea namba badala ya kutoa maelezo anakata Simu... Ila mtu akifanya hivyo nampigia namwambia aache use.nge
 
Kuna ile mtu ana namba 2 kwenye simu yake wew umemtext mfano kwenye voda halaf yeye anajibu na namba ya airtel ambayo huijui na wala hajitambulishi kam mm ni flan huko inakera sana
Hii inakera mno yaani
 
Kuna ile:
My wangu: Vipi baby wafanya nini?
Me: Niko kitandani nataka kulala bb
My wangu: Ahaah sawa mambo mengine vipi bby?
Me: Yako poa vipi huko?
My wangu: Sawa baby mic u mwaaah[emoji849]
Me: Me too luv
My wangu: Asante bby mambo mengine vipi?
Me : Yako poa mpz
My wangu: Mambo yanaendaje lakini?
Me: Tuko poa kwakeli
My wangu: Kwa hiyo ndo unalala bby?
Me: Ndio. Si nimekwambia niko kitandani!.
My wangu: Sawa baby mambo yanaenda vizuri lakini? Unalala zako kwa raha zako

Unaweza kumpigia simu mama, baba yake ukawatukana kwa kuzaa kilaza.
Ukampiga block ya maisha.

[emoji3][emoji3][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] mambo yanaendaje Lakini my wangu?? [emoji28][emoji28][emoji28] usiku unauonaje?
 
Nadhani huu muktadha sio sahihi sana.. linapokuja suala la wapendanao ni tofauti sana, maana yeye anataka kuendelea kuskia sauti yako, kama wewe unaona ni kero, itakuwa humpendi
Hapana aisee hata kama unampenda mtu sio kihivyo bwana....mtu anaanza kukuuliza upo kitandani? Umelala au umekaa? Umevaaje? Umelalaje..kiubavu, chali au umelalia tumbo? Haya maswali huwa hayavumiliki kabisa...hata nikijibu najibu in a way mtu atajua tu kuwa ananikwaza
 
Alikuwa na tabia kunipigia simu usiku wa manani.

Jana ilikuwa siku yake

Leo ananitumia mapicha ya lovebite imebidi avae hijabu ili kuficha
 
Hapana aisee hata kama unampenda mtu sio kihivyo bwana....mtu anaanza kukuuliza upo kitandani? Umelala au umekaa? Umevaaje? Umelalaje..kiubavu, chali au umelalia tumbo? Haya maswali huwa hayavumiliki kabisa...hata nikijibu najibu in a way mtu atajua tu kuwa ananikwaza
Mapenz hayahitaj huo u serious
 
Back
Top Bottom