Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

Hii ni Tabia ya Kiswahili ni ya hovyo na inakera sana

Kumekuwa na matumizi mabaya ya kukera ya simu.

1. Mtu anakupigia simu hujapokea anaendelea kupiga tena na tena. Ukija mpigia baadaye unamuuliza shida nini anakwambia alikuwa anakusalimia tu. Ukiona umepiga simu mara moja mtu hajapokea acha usumbufu. Tulia akiwa Ok atakupigia.

2. Mtu hakudai wala nini anakupigia hupokei anaenda tafuta namba mpya kuendelea kukupigia. Hana jambo la maana anataka mpige stories. Hii tabia ya kukera.

3. Saa nne usiku mtu anakupigia simu mpige stories. Why? Usiku ni muda wa kupumzika wadau heshimu mapumziko ya mwenzio.

4. Mtu anakupigia unamsalimia anakujibu. Then anakwambia "Niambie" inashangaza sana.wewe umenipigia then unataka mimi ndo nikwambie. Nikwambie nini? Ingekuwa na kukwambia ningekupigia.

5. Mtu anakupigia simu kwa namba ngeni unamuuliza nani mwenzangu. Anakwambia ina maana sauti yangu huhifahamu/umeisahau? Huu ni upumbavu, mi sina jukumu la kukariri sauti yako.

6. Kuna wale toka wafahamu whatsapp video call imekuwa nongwa.ikitokea tu kakuona online haraka video call. Huu si ustaarabu. Watu wanataka privacy. Omba kwanza kama its possible kupiga upate kibali.

7. Tabia ya kupiga simu halafu unalalamika. Mbona umekaa muda mrefu hujanipigia simu.ni upuuzi.kama sijakupigia simu ni kwamba sikuwa na cha kukwambia. Kama unacho piga ongea.siyo kuambiana nipe story...

Tutumie simu ipasavyo kama huna cha kuongea na mtu tulia tu. Au salimia kifupi tu basi. Watu tuna mambo mengi kichwani siyo kuleteana habari sizizo na kichwa wala miguu.
Naunga mkono hoja
 
nadhani hiyo namba 7 sio mbaya na inategemeana na wewe na hiyo mtu mna mahusiano gani ? kwa mfano umemaliza weeks hujapiga simu nyumbani kwenu wataacha kukuuliza hivo ? au mpenzi wako
ila kwa jinsi nilivisoma uzi wako mkuu nimegundua wewe ndio umejitakia huo uswahili kwa maana huwezi kuwa na namba za watu wa aina hiyo kama na wewe huna uswahili[emoji23]
 
....ina maana SAUTI YANGU HUIFAHAMU/UMEISAHAU?!!!

Looh[emoji23][emoji23]

IMG_6784.png
 
Mtu anapigiwa simu anasema niko na fulani huyu hapa ongea nae, ningekuwa na shida ya kuongea naye ningepiga mwenyewe simu yake.
 
Hata mtu akimaliza mwezi au mwaka kama unapiga simu unampigia tu si kulaumu kuwa mbona hunipigii kwani kuna makubaliano ya kuwa mimi niwe nakupigia tu?

nadhani hiyo namba 7 sio mbaya na inategemeana na wewe na hiyo mtu mna mahusiano gani ? kwa mfano umemaliza weeks hujapiga simu nyumbani kwenu wataacha kukuuliza hivo ? au mpenzi wako
ila kwa jinsi nilivisoma uzi wako mkuu nimegundua wewe ndio umejitakia huo uswahili kwa maana huwezi kuwa na namba za watu wa aina hiyo kama na wewe huna uswahili[emoji23]
 
Na mimi nina langu.
Unakuta mtu mnafanya kazi pamoja, kuna taarifa muhimu inatakiwa aipate labda kusaini doc fulani ya muhimu. Unampigia simu, unampigia simu hapokei na wala hakuna call back, unaamua kutuma msg nayo kimya hajibu. Unajisemea tu shauri yake! Ishu imetiki na yeye kakosa kwa sababu hakuna sahihi yake, anaanza kukulaumu eti mbona hukuniambia! Una roho mbaya.

Unamwambia lete simu yako nikuoneshe calls zangu na sms nilizotuma. Masikini unakuta kumbe sms hakusoma, hata missed call alizicancel tu na kuendelea na simu mpya tu.

Hii tabia wanayo ndugu zetu wanaoweka simu kwenye pochi, ingawa na wanaume baadhi wanayo hii tabia. Yaani hata ukiwa na shida naye nyumbani, mpaka upige simu ya jirani ndio utaongea naye.

POVU SIO RUKSA.

[emoji1376][emoji1376][emoji1376][emoji1376][emoji1376][emoji1376]
 
GuDume "niambie".....msemo huu wa kishangingi siupendi kweli na mwanamke akinipigia simu na kuanza kusema hili neno nampa red card na kukata kabisa mahusiano naye. Mara nyingi unakuta lishangingi liko na wenzake linakupigia simu na kukuambia niambie mtu wangu ili aonyeshe wenzake kuwa wewe (mwanamme) ni zezeta lake.
 
Na Kuna wale wanaopiga video call mtu Huna no ake wala hujui kama unamfaham au la kisa tu kapata no yako basi ni video call tu ,binafsi sipendi hata kama tumezoeana niambie Kwanza kama naweza pokea au la nakerekwa sana na wenye tabia hizo wengi ni hawa MY wangu
WhatsApp ina setting kuondoa hii kero
Labda tu hujajua kuitumia
 
Ww jamaa inaonekana ni muhaya afu ndio umeanza kushika shika viji hela [emoji3][emoji3]ngoja u broke utatamani hata mtu akubeep
 
Hiyo namba 6 siku hizi kwenye setting kuamua nani akupigie

1. Everyone
2. My Contacts
3. Nobody
 
Kuna ile mtu ana namba 2 kwenye simu yake wew umemtext mfano kwenye voda halaf yeye anajibu na namba ya airtel ambayo huijui na wala hajitambulishi kam mm ni flan huko inakera sana
Kichwa chako kizito tu

Kama ukimtext akajibu hapo hapo unashindwa kuelewa muktadha wa mazungumzo
 
Hapana. Nliambiwa nikaenda mwangalia. Yule hayupo smart kama mimi.mwandiko wake mbaya,una makosa.hana akili za kumwagika.pia si handsome so hata hapati mademu wakali.ingawa kachukua avatar yangu lakin mademu wakienda onana naye live wanamkimbia. Pia nasikia anauzia watu sijui vitabu gani. Mimi Gudume siwezi weka namba yangu kwenye mtandao kwa any business
Kamba hii ni ww ila utaki tuvumbue ukwel !
 
Back
Top Bottom