Hii ni Tanzania ya waswahili. Unaandaaje kumbukumbu ya Hayati Mkapa na kuiendesha kwa lugha ya Kiingereza?

JBITUNGO

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Posts
1,356
Reaction score
613
Nimesikiliza tangu mwanzo kumbukumbu ya Hayati Benjamin William Mkapa. Hii ni Tanzania ya waswahili. Unaandaaje kumbukumbu kama hii na kuiendesha kwa lugha ya kingereza? HAPANA.

Waandaaji wa matukio kama haya kama wa leo UONGOZI INSTITUTE ni vema wakajua kila waandaacho ni kwa ajili ya watanzania na lugha yao ni KISWAHILI.

Asante sana Mhe. Hussein Ally Hassan Mwinyi Rais wa SMZ na baadae Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa JMT kwa kuhutubia hadhara hii kwa lugha ya Taifa Kiswahili.
 
Nawapa hongera sana maana wamewaweka nguvu kazi dakika 50 kwenye traffic!
 
... Mkapa alikipenda na kukiwezea Kiingereza; wacha kumbukizi ya marehemu ifanyike kwa aliyoipenda na kuielewa.
 
Nimesikiliza tangu mwanzo kumbukumbu ya Hayati Benjamin William Mkapa. Hii ni Tanzania ya waswahili. Unaandaaje kumbukumbu kama hii na kuiendesha kwa lugha ya kingereza? HAPANA.

Waandaaji wa matukio kama haya kama wa leo UONGOZI INSTITUTE ni vema wakajua kila waandaacho ni kwa ajili ya watanzania na lugha yao ni KISWAHILI.

Asante sana Mhe. Hussein Ally Hassan Mwinyi Rais wa SMZ na baadae Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa JMT kwa kuhutubia hadhara hii kwa lugha ya Taifa Kiswahili.
Kipindi ha JPM na Kiswahili chake akanangwa kwamba hajui kiingereza...!! Pamoja na yote ila kuthamini cha kwako ndio uungwana.
 
Back
Top Bottom