KWELI Hii ni theluji iliyopo karibu na kilele cha Kibo cha Mlima Kilimanjaro

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari Wakuu,

Nimekutana na video hii TikTok inayodai hii pande kubwa la theluji lipo Mlima Kilimanjaro na lilikuja kutokana na mabadiliko ya Tabianchi. Kuna ukweli hapa?

Naombeni mtusaidie

Your browser is not able to display this video.
---

 
Tunachokijua
Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu zaidi barani Afrika, ukiwa na urefu wa mita 5,895 juu ya usawa wa bahari. Unapatikana kaskazini mwa Tanzania, karibu na mpaka wa Kenya. Kilimanjaro unajulikana kwa kuwa na vilele vitatu: Kibo, Mawenzi, na Shira. Kibo ndicho kilele cha juu zaidi, na ni mahali ambapo mandhari ya theluji ya kudumu inapatikana, ingawa imepungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mlima huu ni kivutio kikubwa cha utalii, na wapanda milima kutoka kote duniani huja kuupanda. Kutokana na mandhari yake ya kipekee, Kilimanjaro pia ni sehemu ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.

Uchunguzi wetu wa awali umebaini kuwa Video hii iliyoletwa na Mdau ilichapishwa na Mnamo Oktoba 5, 2024 na Mtumiaji wa Mtandao wa TikTok aitwaye Abdi Trek ambaye kwenye Bio yake anajitambulisha kama Muongozaji Watalii katika Mlima Kilimanjaro (tazama hapa). Video hiyo yenye dakika 2.43 ameichapisha mara mbili mtawalia, video ya kwanza ni hiyo hapo juu iliyoletwa na Mdau, video ya pili akisisitiza Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na sio Kenya (soma hapa) inaonesha Theruji yenye ukubwa wa kama Bonde kubwa huku ikisindikizwa na sauti inayodai kuwa eneo Hilo ni la Mlima Kilimanjaro linalopatikana karibu na kilele huku hajabainisha ni kilele gani.

Uhalisia wa Video hiyo upoje?
Uchunguzi uliofanywa na JamiiCheck kupitia teknolojia ya Google Reverse Image umebaini kuwa video inayoonyesha bonde kubwa la theluji kwenye Mlima Kilimanjaro ni ya kweli na ilichukuliwa katika mazingira halisi ya Mlima huo. Uhakiki wa picha hizo umetupa video zaidi zinazoonesha wakiwa katika mazingira hayo pamoja na Kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Aidha, katika kupata uhalisia zaidi JamiiCheck imepitia tafiti mbalimbali ambazo zimefanya uchambuzi wa Theruji inayopatikana katika Mlima Kilimanjaro.

ilifanya uchambuzi wa tafiti kadhaa zinazohusiana na theluji kwenye Mlima Kilimanjaro ambazo zinabainisha Picha ambazo zinafanana na video hiyo.

Mathalani, Utafiti Lonnie Thompson (2009), zinaonyesha kuwapo kwa theluji za muonekano huo katika kilele cha Kibo kilicho na urefu wa mita 5,895. Utafiti huo unabainisha kuwa Kibo ndiyo kilele pekee kilichobakia na barafu kati ya vilele vitatu vya Kilimanjaro tazama picha hapa Chini:


Picha ya sehemu ya Kilimanjaro yenye Theruji kubwa iliyowekwa kwenye Utafiti wa Thompson 2009

Theluji Mlima huo itaisha kabisa Mwaka 2035
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa theluji kwenye Mlima Kilimanjaro inaweza kutoweka kabisa kufikia mwaka 2035. Utafiti wa MDPI (2023) umeonyesha kuwa eneo la theluji limepungua kutoka kilomita za mraba 10.1 hadi 2.3 kati ya mwaka 1984 na 2011, ikionyesha kupungua kwa asilimia 77. Aidha, utafiti wa Kaser et al. (2004) unasisitiza kwamba mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile ongezeko la joto na kupungua kwa mvua, yanachangia pakubwa katika kuyeyuka kwa barafu. Utafiti wa Lonnie Thompson pia umeelezea kuwa kati ya mwaka 1912 na 2007, Kilimanjaro ilipoteza asilimia 85 ya barafu yake. Hali hii inatoa taswira mbaya ya hatari inayokabili Kilimanjaro, ikiwa hatua za kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi hazitachukuliwa.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…