Uchaguzi 2020 Hii ni tofauti kati ya kampeni za CCM na CHADEMA

Mati Mkenda

Senior Member
Joined
Mar 4, 2018
Posts
171
Reaction score
211
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia kampeni za vyama hivi viwili ili kujua nini hasa sera zao. Nini hasa watakwenda kutufanyia Watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Ni kwa namna gani watatuletea maendeleo endelevu Watanzania.

Kimsingi nimeona tofauti kubwa sana katika vyama hivi viwili vya siasa. Nimeona tofauti kuanzia namna viongozi wa dini wanavyotoa dua zao hadi wagombea wanavyowasilisha hoja zao. Kiukweli kuna tofauti kubwa sana. Nitaanza kutoa tofauti chache kwa leo.

Dua za Viongozi wa dini. Nimeona kwenye mikutano ya CCM dua inapotolewa na viongozi wa dini kunatawaliwa na hali ya utulivu. Kila mtu aliyepo uwanjani anatulia kwa kiasi kikubwa na dua zinatolewa. LAKINI dua katika mikutano ya Chadema zimejawa na kelele nyingi, makofi, miluzi n.k. Viongozi watoa wa dini wanaotoa dua wamegeuka na kuanza kunadi sera za chama badala ya dua waliyoombwa kutoa, na hadi kufikia hatua ya kuwauliza watu maswali katikati ya dua, na kisha kusubiri majibu kabla ya kuendelea na dua. Nimeona style mpya ya kutoa dua.

Hoja za Wagombea mbalimbali. Katika mikutano ya CCM kumekuwa na mtiririko wa hoja, kwa kuzungumzia wapi tumetoka, wapi tupo, na wapi tunakwenda. LAKINI katika mikutano ya Chadema kumekuwa mihemko mingi, hakuna hoja ya msingi sana, na pengine wagombea wametoa hoja ambazo wananchi wamepiga makofi bila kujua nini hasa wanaambiwa.

  • Mgombea Mwenza Salum Mwalimu anasema, ndege sasa basi, maji sasa basi, barabara sasa basi. Mashabiki wanapiga makofi
  • Mgombea Urais Tundu Lissu anasema, foleni zimekuwa kubwa sana Dar es salaam hasa maeneo ya Gongo la Mboto na Segerea. Watu wanapiga makofi
Tujiulize hawa wawili wanataka nini hasa, kama siyo kujawa na ulaghai mwingi unaotokana na kukosa hoja?
  • Mgombea Urais Lissu anazungumzia Daraja la Baharini kutoka Oysterbay kama halina msaada kwa watu wa Segerea na Gongo la Mboto, lakini haongelei ni kwa namna gani Daraja la Mfugale linawasaidia watu wa maeneo hayo.
  • Mgombea Urais Lissu haongelei tofauti ya miundo mbinu kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya serikali ya awamu ya Tano, na kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya Tano. Wananchi anayowahutubia ni kuwa tangu yeye akiwa Ubelgaji wameacha kuamka saa 10 usiku kama anavyosema yeye. Taarifa zake si sahihi.
  • Mgombea Urais Lissu ameishia tu kuwananga viongozi wa Dini ambao hawajajiweka mstari wa mbele kuunga mkono harakati zao. Kauli zake dhidi ya viongozi wa Dini zimejawa na uongo mwingi, simply tu kuwa anaowaambia si watafuta taarifa.
  • Mgombea wa Ubunge Kawe anasema yeye ni muhuni, mtoto wa mjini; pamoja na lugha kibao za matusi dhidi ya watu wengine. Mashabiki wanapiga Makofi.
  • Lissu anaponda wahujumu uchumi kuomba radhi kwa makosa waliyotenda, lakini anasema ataunda tume kuchunguza yale aliyosema hayaendi sawa nchini, na wahusika watapaswa kuomba radhi. Sijajua anaponda nini na anatuahidi nini cha tofauti. Mashabiki wanapiga Makofi.
Kwa kweli Watanzania tunapaswa kuwa makini sana kusikiliza hoja za wagombea hawa. Tupime kwa makini, ni nini hasa wanatuambia kwamba watakuja kutufanyia.
 
Hao wenye jimbo lao wameelewa ndio maana wakashangilia. Nadhani una tatizo some where.
 
Dua kwenye mikutano ya kampeni hiyo ni kumdhihaki Mungu tu yaani ni sawa na kupiga dua kabla ya disko.

Sifa za mwanasiasa ni
Unafiki
Uongo ulio kisiri
Majigambo yasiyo na maana
Chuki
Roho mbaya

Yaani kwa kifupi siasa ni ushetani mtupu.
 
Dua kwenye mikutano ya kampeni hiyo ni kumdhihaki Mungu tu yaani ni sawa na kupiga dua kabla ya disko.

Sifa za mwanasiasa ni
Unafiki
Uongo ulio kisiri
Majigambo yasiyo na maana
Chuki
Roho mbaya

Yaani kwa kifupi siasa ni ushetani mtupu.
Watakuelewa wachache. Sometime nahisi jamii iko demonic, maana si kwa mihemuko hii.
 
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM hata akinywa maji jukwaani 'Mazuzu' yanapiga makofi na kushangilia
 
Watanzania watawapimaje wagombea wakat walio wengi hawana elimu..

Nyumba kwenu wenye mawazo na uwelewa kama wakwako wako wangapi ,ukiona mko wachache ujue bado washangiliaji niwengi
 
Mgombea wa chadema sasa anaenda na upepo, ikifika usiku anaingia hum JF na kusoma mawazo ya watu kisha ana andaa hoja ya kusema kesho yake

Kwa hiyo tutegemee kudanganywa sana kwa sababu hakuna dhamila ya dhati aliyonayo tofauti na kutaka kumtoa magufuli tu.

Nadhani chama bado hakijaanda ilani yao kama mwaka 2015 hivyo wanategemea watu wanasema nini kwenye mitandao
Kisha wana copy na kuyalekebisha na kuingia nayo jukwaani.
 
Ninachompendea Lissu kila akimtaja JPM huwa anaanza na "muheshimiwa Rais Magufuli"hii inaonyesha ni jinsi gani JPM ananafasi ndani ya moyo wa Lissu.
 
Mkuu upinzani hawana hoja cheki hata hapa JF huwa mara nyingi hawajibu hoja. Sasa subiri uone mapovu.
Mkuu una uhakika sisi wapenzi na washabiki wa upinzani hatuna hoja?
We dogo unaweza shindana nasi kwa hoja,ukatushawishi ???

Tofauti Ni kuwa sisi hatulipwi, hatuko njaa oriented tuko rational na hatuko biased
 
Mkuu ulivyoanza uzi wako ilikuwa kama unataka kuleta tofauti ya ccm na cdm. Paragraph za mwanzo ulitaka kujaribu, lakini kwa kadiri ulivyosogea ukawa hutoi tofauti baina ya vyama hivyo viwili, bali ukawa unaongea unavyokwazika na kampeni za cdm. Nikushauri kitu, waombe mods wabadili heading isiwe tofauti ya kampeni za cdm na ccm, bali iwe kampeni za cdm zinavyokukwaza. Huna tofauti na makada wenzako wa ccm kwa maudhui, bali tofauti yako ni kuandika kwa kuzingatia matumizi ya koma, nukta na kuweka paragraphs fullstop.
 
Mkuu una uhakika sisi wapenzi na washabiki wa upinzani hatuna hoja?
We dogo unaweza shindana nasi kwa hoja,ukatushawishi ???

Tofauti Ni kuwa sisi hatulipwi, hatuko njaa oriented tuko rational na hatuko biased
Mngekuwa hamna njaa viongozi wenu wangekuwa wananunuliwa kama njugu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…