Mati Mkenda
Senior Member
- Mar 4, 2018
- 171
- 211
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia kampeni za vyama hivi viwili ili kujua nini hasa sera zao. Nini hasa watakwenda kutufanyia Watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Ni kwa namna gani watatuletea maendeleo endelevu Watanzania.
Kimsingi nimeona tofauti kubwa sana katika vyama hivi viwili vya siasa. Nimeona tofauti kuanzia namna viongozi wa dini wanavyotoa dua zao hadi wagombea wanavyowasilisha hoja zao. Kiukweli kuna tofauti kubwa sana. Nitaanza kutoa tofauti chache kwa leo.
Dua za Viongozi wa dini. Nimeona kwenye mikutano ya CCM dua inapotolewa na viongozi wa dini kunatawaliwa na hali ya utulivu. Kila mtu aliyepo uwanjani anatulia kwa kiasi kikubwa na dua zinatolewa. LAKINI dua katika mikutano ya Chadema zimejawa na kelele nyingi, makofi, miluzi n.k. Viongozi watoa wa dini wanaotoa dua wamegeuka na kuanza kunadi sera za chama badala ya dua waliyoombwa kutoa, na hadi kufikia hatua ya kuwauliza watu maswali katikati ya dua, na kisha kusubiri majibu kabla ya kuendelea na dua. Nimeona style mpya ya kutoa dua.
Hoja za Wagombea mbalimbali. Katika mikutano ya CCM kumekuwa na mtiririko wa hoja, kwa kuzungumzia wapi tumetoka, wapi tupo, na wapi tunakwenda. LAKINI katika mikutano ya Chadema kumekuwa mihemko mingi, hakuna hoja ya msingi sana, na pengine wagombea wametoa hoja ambazo wananchi wamepiga makofi bila kujua nini hasa wanaambiwa.

- Mgombea Mwenza Salum Mwalimu anasema, ndege sasa basi, maji sasa basi, barabara sasa basi. Mashabiki wanapiga makofi
- Mgombea Urais Tundu Lissu anasema, foleni zimekuwa kubwa sana Dar es salaam hasa maeneo ya Gongo la Mboto na Segerea. Watu wanapiga makofi
- Mgombea Urais Lissu anazungumzia Daraja la Baharini kutoka Oysterbay kama halina msaada kwa watu wa Segerea na Gongo la Mboto, lakini haongelei ni kwa namna gani Daraja la Mfugale linawasaidia watu wa maeneo hayo.
- Mgombea Urais Lissu haongelei tofauti ya miundo mbinu kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya serikali ya awamu ya Tano, na kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya Tano. Wananchi anayowahutubia ni kuwa tangu yeye akiwa Ubelgaji wameacha kuamka saa 10 usiku kama anavyosema yeye. Taarifa zake si sahihi.
- Mgombea Urais Lissu ameishia tu kuwananga viongozi wa Dini ambao hawajajiweka mstari wa mbele kuunga mkono harakati zao. Kauli zake dhidi ya viongozi wa Dini zimejawa na uongo mwingi, simply tu kuwa anaowaambia si watafuta taarifa.
- Mgombea wa Ubunge Kawe anasema yeye ni muhuni, mtoto wa mjini; pamoja na lugha kibao za matusi dhidi ya watu wengine. Mashabiki wanapiga Makofi.
- Lissu anaponda wahujumu uchumi kuomba radhi kwa makosa waliyotenda, lakini anasema ataunda tume kuchunguza yale aliyosema hayaendi sawa nchini, na wahusika watapaswa kuomba radhi. Sijajua anaponda nini na anatuahidi nini cha tofauti. Mashabiki wanapiga Makofi.