Hii nime copy pahala

Hii nime copy pahala

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
C&P
Rais @SuluhuSamia , haya anayoyaongea Rais @WilliamsRuto ndiyo tunayotaka kuyasikia kutoka kwako, sio mahubiri ya dini.

Tunataka kusikia umekataa kuidhinisha bajeti ya Bilioni 180+ kuhudumia wabunge 390 pale Dodoma huku umma wa watanzania ukiteseka na umaskini uliokithiri.

Tunataka kusikia umekataa kuidhinisha bajeti ya Bilioni 190+ kununulia viongozi V8 huku umma wa watanzania ukikosa uhakika wa miło miwili tu kwa siku.

Tunataka kusikia umesitisha ongezeko la mishahara na posho za wabunge ambao wanakunja zaidi milioni 16 kwa mwezi na milioni 200 za gratuity kila miaka mitano; hatukuchagua watu kutunyonya kiasi hiki.

Tunataka kusikia umesitisha malipo ya posho kwa wenza wa viongozi; hawa watu wanaupa mzigo umma wakati tayari wameshachuma mali za umma siku zote za utendaji wao, huu ni zaidi ya wizi.

Tunataka kusikia umesitisha bajeti za matumizi ya hovyo kwenye ofisi ya Rais na Wizara ya Mambo ya Nje ambazo zinachezea pesa za umma kumsafirisha Rais na wapambe wake nchi za nje kwa ndege binafsi kila leo na kufanya warsha ikulu kila mara.

Tunataka kusikia umesitisha matumizi ya mabilioni ya kodi za watanzania maskini kugharamia misafara yako na ya viongozi wa CCM kila leo huku umma ukiteseka kwa kukosa social services.

Tunataka kusikia umeondoa bajeti za kugharamia mambo yasiyokuwa na tija kwa umma kama mbio za mwenge na maadhimisho ya sherehe za kitaifa zisizokuwa na ulazima.

Tunataka kusikia wabadhirifu wote kwenye report za CAG wakifanyiwa kazi na fedha za umma zilizoibiwa zikirudishwa.

Tunataka kusikia mijadala ya sababu za kukopa kwenye taasisi za kimataifa na umma kuridhia mikopo hiyo kabla ya kwenda kukopa. Tumechoka kubebeshwa mzigo wa kuhudumia deni la taifa huku wanaoneemeka na fedha za mikopo mkiwa ninyi na familia zenu.

Tunataka kusikia vipengele vya mikataba ya kimataifa vimewekwa wazi na kujadiliwa na umma kabla ya kusainiwa. Tumeshajifunza mengi kutoka kwa IPTL na ESCROW; tunajua pia hii mikataba inasainiwa baada ya viongozi kulipwa pesa nyingi za rushwa na kuahidiwa kickbacks, ni muda wa umma kusimamia maslahi yake.

Tunataka kusikia mgawanyo mpya wa majimbo ya uchaguzi unaozingatia idadi ya watu wanaowakilishwa na uwezo wa uchumi wetu. Tuna bunge kubwa lenye wabunge walioingia bungeni kwa kura mpaka elfu moja, kugharamia huu mzigo ni matumizi ya hovyo yanayouumiza umma.

Tunataka kusikia hizi fedha zikielekezwa kusubsidize bima ya afya ya Toto Afya Kadi ambayo watoto wa watanzania maskini wameporwa.

Tunataka kusikia hizi fedha zikielekezwa kwenye projects za kuujengea uwezo (re-skilling and up-skilling) umma wa watanzania ambao ni functionally illiterate kwa zaidi ya asilimia 80%.

Tunataka kusikia hizi fedha zikielekezwa kwenye mfuko wa vijana na kutoa mikopo kwa vijana wengi ambao hivi sasa wamegeuka kuwa wateja wa pombe, kamari, na biashara ya ukahaba.

Haya na mengine mengi ya aina hii ndiyo tunayotaka kusikia kutoka kwa Rais, sio kukwepa uwahi ilani na kujificha nyuma ya mawaisha ya dini na maadili.
 
Back
Top Bottom