cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 498
Weee sema chochote upendacho kuhusu hii picha lkn mie imenikumbusha mbali sana back to 80's wakati niko mtoto, hasa wakati wa xmas mama yetu alikuwa ananunua kitambaa cha aina moja wote kuanzia dada zangu hadi mimi tunashonewa kitambaa hicho hicho hadi mshono mmoja.
Viatu mnanunuliwa vikubwa kidogo eti ili ukuwe navyo mbele unajazia na karatasi ili vitoshe.
mkishakula pilau na double cola mnapewa hela muende mjini mkatembee,basi nilikuwa najiona nimependezaa,usoni mmepakwa mafuta ya rays mnang'aa kama kioo.
Mkienda kutembea mjini mtu unatembea kama kiwete maana viatu vinaumiza..aah nafurahi kuwa mtu mzima maana leo hii nisivyopenda nguo za kushona.leo nikiamua kuvaa leging na skin jeans hakuna wakunichagulia.
Utu uzima raha jamani.