Hii picha ya Bill Gates na familia nchi zinazoendelea imenitafakarisha sana

Ndivyo maisha yalivyo, elimu elimu elimu ndio silaha kuu ya kumtoa huyo mwananchi kutoka hali aliyonayo. Pia, watu wengi wanaishi maisha waliyonayo kwani wameridhika na hali zao, no need of hustling, wamekata tamaa na kuona ni maisha ya kawaida tu.

Uwepo wa watu kama Bill gate na huyo mwananchi ndio unaleta raha ya maisha na ugumu au karaha ya maisha, yupo anafurahi kuona mwingine akiishi maisha kama hayo japo nayeye huyo anaumia na kutamani kufikia hatua kama ya Gate.

Maisha muda mwingine yanaumiza na kukatisha tamaa mwisho wa siku wivu, roho mbaya na hata kuoneana aibu inaanzia hapa .



Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Exposure pia inasaidia, unajua zamani enzi za ukoloni vijijini kulikuwa na jumba la maendeleo wananchi walifanya disco na kuangalia filamu mwisho wa wiki. Hata mwanzo wa Ujamaa hizi nyumba zilikuwepo. Mkiwaonyesha documentaries za wanaoishi nyumba zenye standaard ya juu kidogo wataiga.

Mzungu alifanikiwa sana kutugawa Africa, kama tungekuwa na soko huru la bidhaa zetu ndani ya Africa soko lingekua kubwa kwani tunakula vyakula karibu sawa, mihogo, majimbi, ndizi, matunda.
 
watu walioendelea hawanaga makuu, makuu wanayo wenye vijisent wao kutwa ni show off nakutaka kila mtu awajue.
 
Hiki kijiji kinaitwa kicheba kipo wilayani Muheza ,ardhi yake ni maarufu kwa kilimo cha mihogo aina ya kibanda meno
 
Sio lushoto hapo panaitwa kicheba Muheza mkoa wa Tanga, picha ilipigwa alipokuja kwenye project ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele mabusha na matende
 
Huo ni utetezi wa kijinga sana !!!kwani kina nchi ngapi za Asia zilitawaliwa na Leo zipo mbali???? Kwa kifupi tuu waafrika hatuwezi kujitawala na kujiletea maendeleo
 
Kuwakomboa kivipi? Kwa kulima na jembe la mkono?
 
Muheza hio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…