Hii sasa ni Dharau kwa MaMiss wetu....

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Angalia hii zawadi ya Miss Kanda ya Ziwa 2018 (Miss Lake Zone) ifike wakati sasa tuache kuwadhalilisha mabinti zetu tunaua morali na vipaji kwa upuuzi kama huu....#WTF
UPDATES
==============
Baada ya Picha ya gari kimeo kwa ajili ya zawadi ya miss kanda ya ziwa kusambaa mitandaoni....

Waandaaji wa Miss Tanzania, The Look Company kupitia kwa Mkurugenzi wake Basilla Mwanukuzi wameikataa zawadi hiyo ya gari aina ya Passo yenye thamani ya shilingi Milioni 8,kwa mujibu wa Mwanukuzi amesema wameandikia barua waandaaji wa Miss Lake Zone kuwa wabadilishe zawadi hiyo huku nakala ya barua hiyo pia ikipelekwa BASATA.

Mwanukuzi amesema waandaaji wadogo wadogo wa mashindano kama hayo hawana ulazima wa kutoa zawadibkubwabkubwa na badala yake wanatakiwa kuwaandaa na kutafuta warembo kwa ajili ya mashindano makubwa ya Kitaifa.

Mashindano hayo ya miss Lake Zone yanatarajia kufanyika keshoJumamosi, august 4,jijini Mwanza.
 
Wapokeaji wasuse wasikubali kuchukua gari hiyo kisu hicho kitamuua mtumiaji bora kuacha kabisa kuliko kupokea tetenasi hiyo
Halafu na wao walivyo wajinga wamekubali kupigwa picha mbele ya hako kagari screpa....
 
Hata zawadi ya siku ya Birth Day Inaafadhali kwa watu fulani hivi.....!


Kama vile vigali vya oLd skul "Mgongo chura" vitaili vya toyo

mi nahisi Zawadi hizi zinakuwa based na location, ulitoka kusini zawadi zinakuwa ugly na hovyo, ukitoka juu kaskazini unakuwa na thamani we look back mashindano yaliyopita
 
Wapokeaji wasuse wasikubali kuchukua gari hiyo kisu hicho kitamuua mtumiaji bora kuacha kabisa kuliko kupokea tetenasi hiyo
labda aseme aombe pesa yenye thamani ya hako ka gari na sijui kama watakubal
 
Wasipojipa thamani wao wenyewe,wasahau kuheshimiwa,
Siku zote maisha hukupa unachostahili,sio unachotaka,ma miss wetu wengi,SUBCONCIOUSLY,wanaamini hata kuchaguliwa kushiriki,ni hisani,mpaka pale watakapojua thamani yao,wataendelea kuchezewa hivi hivi,kwenye kamati za majizi,viongozi ni wanaume,hivi ngazi za juu za timu ya Yanga na Simba,viongozi wanawake ni wangapi?,
Ukitaka kilicho bora,raise ur standard,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…