Hii sheria inaniumiza moyo, ufafanuzi tafadhali

Hii sheria inaniumiza moyo, ufafanuzi tafadhali

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
573
Reaction score
140
Habarini, nilipata mtoto miaka 9 iliyopita bila kufunga ndoa na baba wa mtoto. miaka 5 baadae alifunga ndoa na mwanamke mwingine. lakini tangu nipate ujauzito matumizi ya mtoto yalitolewa kwa nadra sana, mara baada ya baba mtoto kufunga ndoa matumizi yalipungua na hatimaye kuisha kabisa. sasa ni takribani mwaka na nusu sina mawasiliano na baba mtoto. sheria inasema kuwa mtoto ana haki ya kuchukuliwa na babaye mara afikishapo 7 years.namgharamia sana kiasi kwamba naumia kujua ipo siku atachukuliwa na babaye
https://www.jamiiforums.com/login.php?do=login
 
je mimi mama wa mtoto nina haki ya kuishi na mtoto? je kama baba wa mtoto akitaka kumchukua vipi kuhusu gharama na matumizi ya mtoto. naomba msaada wenu wanasheria. asanteni
 
Anatakiwa kupata matunzo kutoka kwa baba wa mtoto kila mwezi ili mradi ithibitike huyo ni mtoto wa mtuhumiwa wako.
Atapa matunzo mpaka afikishe miaka 18. kwanza nenda kwenye offisi za ustawi wa jamii kwanza utapata msaada. Ukikosa hapo una kwenda mahakamani.

Lakini kwenye swala la mirathi anaweza asihusike. Huyo ni mtoto haramu= out of weddlock child
 
Sababu ni mtoto wa nje ya ndoa na amesha zidi miaka saba bila shaka ana huwezo wa kuchagua anataka kuishi na nani.

Kisheria baba huyo hawezi kulazimisha kukaa nae kama mtoto hataki na matunzo ataendelea kutoa kama kawaida.

Hivyo usiogope we fata sheria tu utapata haki yako. Na mtoto ndio ataamua ana taka kukaa na nani
(castody and mantainance of children).

Usijali sheria itafatwa na kila mtu kati yenu ana haki ya kukaa na mtoto huyo.
je mimi mama wa mtoto nina haki ya kuishi na mtoto? je kama baba wa mtoto akitaka kumchukua vipi kuhusu gharama na matumizi ya mtoto. naomba msaada wenu wanasheria. asanteni
 
duh, akimchukua unatamani akulipe pesa ulizotumia kumtunza??

Na kwa nini unadhani atamchukua? Huko aliko hana watoto wengine?

Pesa ya matumizi kisheria ni ndogo sana, huhitaji hata kuidai, labda sh.100 kwa siku, ya nini sasa? Hata kama ni 1,000 kwa siku.
 
Ruttashobolwa asante kwa ufafanuzi, kabla hatujakata mawasiliano alikuwa anasisitiza kuwa mimi nimpeleke mtoto amsalimie / amwone kumbuka kuwa hajawahi kumwona miaka yote 9. nikimwambia aje amwone nyumbani anadaia anamwogopa mama yangu kisa aliwahi kujibishana kwa simu kipindi cha nyuma, hivyo hajawahi kumwona kwa macho zaidi ya picha za passport size. pia anadai kwa mila za kwao inatakiwa mimi mama wa mtoto kumpelekea mtoto na sio yeye baba wa mtoto kuja kumwona. kwa hiyo ndio akaamua kukata mawasiliano
 
Last edited by a moderator:
Peleka huyo chizifresh ustawi wa jamii. Umpelekee mtoto ni parcel hiyo? Muambie utampost siku moja kwa dhl, atoe hiyo hela. Ovyooo!
 
Mi nitajikita kwenye swala la matunzo ya mtoto ni haki ya mtoto kupata matunzo kutoka kwa baba.
Je ulishawai kumuomba pesa za matunzo ya mtoto?
Swala la kwenda kumsalimia au kumpeleka aka msalimie ni makubaliano yenu wawili. Lakini kumbuka huyo baba ana haki kumuona, lakini kama ata kutumia nauli umpeleke kumuona sioni tatizo. Unatakiwa uhakikishe mtoto ana pata matunzo ndio maana nikashauri uende offisi za ustawi wa jamii!

Nina cho jiuliza wewe ulikata mawasiliano au yeye alikata mawasiliano? Maana kwa hapa hata yeye anaweza kujitetea .
Ruttashobolwa asante kwa ufafanuzi, kabla hatujakata mawasiliano alikuwa anasisitiza kuwa mimi nimpeleke mtoto amsalimie / amwone kumbuka kuwa hajawahi kumwona miaka yote 9. nikimwambia aje amwone nyumbani anadaia anamwogopa mama yangu kisa aliwahi kujibishana kwa simu kipindi cha nyuma, hivyo hajawahi kumwona kwa macho zaidi ya picha za passport size. pia anadai kwa mila za kwao inatakiwa mimi mama wa mtoto kumpelekea mtoto na sio yeye baba wa mtoto kuja kumwona. kwa hiyo ndio akaamua kukata mawasiliano
 
Last edited by a moderator:
Ruttashobolwa, matumizi alikuwa anatoa kwa nadra sana. anaweza kutuma sh.20000 - 50000 kila baada ya miezi mitatu. ama asitume kabisa. na alipooa ndo matumiz yalisitishwa kabisa.kuhusu mawasiliano yeye ndo alikata kwani ilifika kipindi nikimpigia hapokei,nikituma sms hajibu. nikitumia simu tofauti akipokea akasikia ni mimi anakata simu. nikaamua bora nikae kimya. Ndio ana haki ya kumuona lakini haileti maana mimi nifunge safari kwenda kwake wakati ana family. AU NI SAWA KWENDA KWAKE?je mkewe atanielewaje
 
Last edited by a moderator:
Ok! Alitakiwa atoe kila mwezi si chini ya 15,000 kwahiyo alitakiwa ahakikishe ana zitoa hizo pesa kama matumizi.

Unajua kama ata kutumia nauli ni bora uende ili uweze kupata haki za mtoto kirahisi kwani utashindwa kupata haki za mtoto kirahisi kama utakuwa mbali na mtuhumiwa!
Ok kama una uwezo wa kumlea mwanao bila kuhitaji msaada ni sawa japo ni lazima!

Kama ana hitaji kumuona mtoto mwambie aje kumuona au kama ata kutumia nauli usisite hili uweze kupata haki za mwanao vizuri, kwani hata ukienda ustawi wa jamii au mahakamani baba ata hitajika kutoa maelezo na kuambiwa cha kufanya!

Na kama utafunga safari kwenda kumpeleka mtoto unaweza kufikia kwenye nyumba ya wageni. Au kama uoni haja ya kumpeleka yeye mwenyewe aje!

Ruttashobolwa, matumizi alikuwa anatoa kwa nadra sana. anaweza kutuma sh.20000 - 50000 kila baada ya miezi mitatu. ama asitume kabisa. na alipooa ndo matumiz yalisitishwa kabisa.kuhusu mawasiliano yeye ndo alikata kwani ilifika kipindi nikimpigia hapokei,nikituma sms hajibu. nikitumia simu tofauti akipokea akasikia ni mimi anakata simu. nikaamua bora nikae kimya. Ndio ana haki ya kumuona lakini haileti maana mimi nifunge safari kwenda kwake wakati ana family. AU NI SAWA KWENDA KWAKE?je mkewe atanielewaje
 
Last edited by a moderator:
Mwisho wa siku mtoto atadai umwonyeshe baba yake.
Nadhani huwa udhawahi kusikiliza vle vpindi vya kutafutana.
 
Back
Top Bottom