Nyakwaratony
JF-Expert Member
- Dec 21, 2011
- 573
- 140
Habarini, nilipata mtoto miaka 9 iliyopita bila kufunga ndoa na baba wa mtoto. miaka 5 baadae alifunga ndoa na mwanamke mwingine. lakini tangu nipate ujauzito matumizi ya mtoto yalitolewa kwa nadra sana, mara baada ya baba mtoto kufunga ndoa matumizi yalipungua na hatimaye kuisha kabisa. sasa ni takribani mwaka na nusu sina mawasiliano na baba mtoto. sheria inasema kuwa mtoto ana haki ya kuchukuliwa na babaye mara afikishapo 7 years.namgharamia sana kiasi kwamba naumia kujua ipo siku atachukuliwa na babaye
https://www.jamiiforums.com/login.php?do=login
https://www.jamiiforums.com/login.php?do=login