Nyakwaratony
JF-Expert Member
- Dec 21, 2011
- 573
- 140
je mimi mama wa mtoto nina haki ya kuishi na mtoto? je kama baba wa mtoto akitaka kumchukua vipi kuhusu gharama na matumizi ya mtoto. naomba msaada wenu wanasheria. asanteni
Ruttashobolwa asante kwa ufafanuzi, kabla hatujakata mawasiliano alikuwa anasisitiza kuwa mimi nimpeleke mtoto amsalimie / amwone kumbuka kuwa hajawahi kumwona miaka yote 9. nikimwambia aje amwone nyumbani anadaia anamwogopa mama yangu kisa aliwahi kujibishana kwa simu kipindi cha nyuma, hivyo hajawahi kumwona kwa macho zaidi ya picha za passport size. pia anadai kwa mila za kwao inatakiwa mimi mama wa mtoto kumpelekea mtoto na sio yeye baba wa mtoto kuja kumwona. kwa hiyo ndio akaamua kukata mawasiliano
Ruttashobolwa, matumizi alikuwa anatoa kwa nadra sana. anaweza kutuma sh.20000 - 50000 kila baada ya miezi mitatu. ama asitume kabisa. na alipooa ndo matumiz yalisitishwa kabisa.kuhusu mawasiliano yeye ndo alikata kwani ilifika kipindi nikimpigia hapokei,nikituma sms hajibu. nikitumia simu tofauti akipokea akasikia ni mimi anakata simu. nikaamua bora nikae kimya. Ndio ana haki ya kumuona lakini haileti maana mimi nifunge safari kwenda kwake wakati ana family. AU NI SAWA KWENDA KWAKE?je mkewe atanielewaje