Hii show ya Fally Ipupa, Kinshasa itaweka rekodi ambayo haitavunjwa kirahisi.

Hii show ya Fally Ipupa, Kinshasa itaweka rekodi ambayo haitavunjwa kirahisi.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu nimesoma mitandaoni kuhusu show ya Fally Ipupa huko kwao Kinshasa nikabaki kinywa wazi. Huyu jamaa yuko serious. Hakuna longolongo. Yaani pamoja na kufanya promo kwa mbinu zilizozoeleka lakini kijana akaamua kukodi ndege kadhaa kwa ajili ya kutangaza show mjini Kinshasa. Tazama picha jinsi walivyoripoti Congo Bleu.

Na leo tarehe 29/10/2022 kufika saa 9 alasiri tayari uwanja ulikuwa umejaa umati ukisubiri show ianze saa 1 jioni. Cha kushangaza pia kaweka kapeti pale kwenye Pitch ili kuzuia uharibifu. Kwenye Insta ya Dacota wa Clouds kuna video katuonyesha.

Hili ni somo kwa wadau wote wa muziki nchini. Nadhani Dacota akirudi atasimulia vingi.
 

Attachments

  • FB_IMG_1667061182396.jpg
    FB_IMG_1667061182396.jpg
    103.8 KB · Views: 12
  • Screenshot_20221025-193521_Facebook.jpg
    Screenshot_20221025-193521_Facebook.jpg
    83.9 KB · Views: 10
  • FB_IMG_1667062208103.jpg
    FB_IMG_1667062208103.jpg
    58.1 KB · Views: 10
Huyu jamaa natamani sana siku moja kushuhudia show yake
 
Back
Top Bottom