Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Miezi mitatu iliyopita, Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, aliweka wazi kuwa kikosi chake hakikuwa kimefikia kiwango cha ushindani asilimia 100. Alipoulizwa hivi karibuni kuhusu maendeleo ya timu kwa neno moja, jibu lake lilikuwa "MAENDELEO."
Akizungumza kwa kina, Davids amesema:
"Tulikipata kikosi tukiwa hata siyo sifuri, bali hasi -5. Hii ilitokana na wachezaji waliokuwa nje ya mazoezi kwa wiki nane, huku wengine wakiwa na changamoto kubwa katika maandalizi ya msimu mpya. Tulianza taratibu na kwa hatua kwa hatua tukajenga utimamu wa mwili sambamba na misingi ya aina ya uchezaji ninaoutaka.
"Uchezaji wetu unahitaji ukali mkubwa, nguvu nyingi, kukaba kwa ustadi, na kushambulia wapinzani bila kuchoka. Hatuna budi kuwa na misingi imara ya kimchezo ili kufanikisha haya yote. Kutoka siku ya kwanza hadi sasa, tumepiga hatua kubwa. Hata hivyo, bado hatujafikia uwezo kamili wa kikosi, lakini tunaendelea kwa mwelekeo sahihi."
Bila shaka Mashabiki wa Lunyasi mnaendelea kushuhudia hatua za kujengwa kwa kikosi chenye ushindani wa hali ya juu msimu huu au mnasemaji?
Video: dicksonjackson