Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tulimsikia Rais wetu, Samia Suluhu Hassan, katika hotuba yake ya majuzi, huko Katika Chuo cha Polisi
Moshi, akieleza kuwa baadhi ya maofisa wa Polisi, wanaiba mafuta ya petrol/diesel, wanayoletewa kwa matumizi ya Umma na kuyaweka kwenye daladala zao binafsi!
Rais Samia pia akaendelea kueleza kuwa taarifa anazo, hadi namba za hayo magari binafsi "yanayokunywa" hayo mafuta yetu yaliyotengwa kwa matumizi ya Umma.
Swali kubwa ninalomuuliza Rais wetu ni hili, ikiwa yeye ametuthibitishia kuwa hadi namba za hayo magari binafsi za hao makamanda anazo, je ni kwanini anashikwa na kigugumizi na hachukui hatua kwa makosa hayo ya dhahiri ya jinai?
Hivi Rais wetu anajisikiaje anapoona maelfu ya wahalifu wengine wa makosa madogo madogo, kama vile wezi wa kuku, wakitupwa magerezani kila uchao, kwenye Mahakama zetu hapa nchini, wakati hao makamanda wa Polisi akiwaachia watembee huru uraiani?
Huu ubaguzi wa wazi kabisa wa kuwafanya baadhi ya wananchi kuwa na "impunity" na kutoweza kushitakiwa na wengine wawe wanaozea jela kwa makosa madogo madogo, siyo "fair" kabisa