Hii tabia ni mbaya sana kwa baadhi ya wanaume wa JamiiForums. Kupewa namba sio lazima

Hii tabia ni mbaya sana kwa baadhi ya wanaume wa JamiiForums. Kupewa namba sio lazima

kadogo2

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
1,889
Reaction score
3,059
Kwanza kabisaa usiamini story zote humu utakuwa mjinga sana humu kuamini kila story na kuanza kumdefine mtu kulingana na story alioleta… visa vingi ni uongo uongo

Hii tabia imekuwa kero sana kwa watu wa humu jf (wanaume),, lengo la kutumia ID fake ni ili mtu alete kisa chake na majanga yanayo msibu bila kutambulika na yoyote yaani mtu anakuwa huru kutoa ya moyoni mwake

Wakati mwinginee pia hivi visa havina uhalisia ni kuchangamsha genge la JF na mtoa story kupunguza stress anapoingia humu

Sasa nashindwa kuwaelewa wale wanakimbilia PM kuomba namba tena kwa ulazima… mtu unakuta unamwambia nishauri humuhumu ila anabaki kukulazimisha utoe namba.. huwa nawashangaa mnataka cha ziada nini… tutoe namba zetu humu ili identity zenu zijulikane na wengine mlivyo wa hivyo muje mututangaze humu

Mimi niliacha hadi kutumia ID yangu ya zamani kwasababu kuna baadhi ya watu nilikosea sana nikawapa namba yangu na tumekuwa marafiki na story nazozileta humu hazifanani na uhalisia wa maisha wangu kwa mitazamo yao so ikawa ngumu mimi kuandika visa vyangu kwa ID yangu ikabidi nitengeneze ID mpya

Mwinginee anakuja PM anakwambia ameona Mimi nafaa kuwa mke wake mpk unaanza kujiuliza huyu ana wazimu hatujuani sikujui na huna uhakika kama hii ID ni ke o me ila umekazana kusema tunaendana huwa mnakuwa na wendawazimu kichwani mwenu

Kama mtu kaomba ushaurii hajasema kuwa anahitaji kutoa mawasiliano yake na hajapost kutafuta mume au mke kwenye jukwaa la Love connect muache jamani kutusumbua

Wengine hatuwezi kuzifunga hizo pm kwasababu kuna baadhi ya member wanashindwa kuchangia mada labda for their reasons wanaamua kuja pm ili kutoa ushaurii

Mawasiliano hayalazimishwi jamani kama nimeomba ushaurii unaweza kunishauri bila Kutaka namba yangu.. kama ningehitaji kujulikana basi platform ni nyingi na wana saikolojia ni wengi ningeenda huko kuomba ushaurii

Nipo jf kuomba ushaurii wowote kwasababu ni sehemu ambayo ninajisikia comfortable kueleza chochote bila kujulikana na yoyote humu

Haya ninayasema kwasababu kuna members wamekuwa wakinishambulia PM kwa maneno mabaya kisa tu nimekataa kutoa namba yangu… jambo ambalo limeniudhi.. kama mtu kisa namba anaweza kunitolea maneno machafu hata nikimpa namba yangu hashindwi kuja kuni expose humu

Tuheshimiane humu.. hizi story za humu zinaishiaga humu na story zingine nyingi humu ni Chai tu hazina uhalisia… sasa wewe kujifanya una ushaurii sana mpk kulazimisha namba na ukinyimwa unaleta matusi hebu huo ushaurii jishauri mwenyewe labda utakusaidiaa

Weekend njema
 
Kuna member alianzisha uzi juzi kati akiomba namna ya kukwepa zawadi sijui na blah blah kama hizo nikamuuliza kama alishawahi kusikia neno SITAKI

Na wewe kama hujawahi kusikia neno SITAKI basi nakuelekeza....maana yake ni kukataa,litumie hilo huko PM,litakusaidia
 
Kwanza kabisaa usiamini story zote humu utakuwa mjinga sana humu kuamini kila story na kuanza kumdefine mtu kulingana na story alioleta… visa vingi ni uongo uongo
Tukianza na wewe wewe siyo wa kike wewe ni wa kiume na inakera sana mtoto wa kiume ku-act uanamke.

Mtoto wa kiume kutunga story kwamba sometimes huwa anafurahia uume siyo jambo la maana hata kidogo aloo acha hizo.
 
Wape tu namba mkuu
Hupungukiwi na chochote. Kutoa namba sii kutongozwa au kujulikana. Abduli anaweza kukuomba namba humu ukakosa opportunity.
Pia usipopenda kua na namba za mtu humu ni haki yako pia.
financial services na mimi tumekua marafiki humu kwa miaka kadhaa lkn sijaomba namba za simu(🤣Bado)
 
Mtoa mada Sasa. 😆😂😂
FB_IMG_17368499995570923.jpg
 
Sasa kwa nini ulete fictitious story huku unaeleza namna unavyopitia changamoto fulani, unategemea sisi tukuelewe vipi?

Kumbuka watu wanatumia resources zao za muda na kuwaza namna gani watakushauri uondokane na hilo janga.

Fikiria mtu analeta story ya namna anavyopambana na maisha, amekata tamaa na anataka kujiua/kufa. Unatoa ushauri na badae unakuja kufahamu jamaa alikuwa anatania, unajisikiaje?
 
Story za JF sio za kuzichukulia serious, humu kila mtu anapiga goli 5, kila mtu ana mwanamke mkali, kila mtu anamiliki gari, kila mtu ana nyumba kali, kila mtu ana degree na amesoma UDSM, kila mtu alipata division 1 form 4 na six na ana GPA kali.
 
Ni totally bullshit
 
Bro mimi ni raisi wa ma jobless pro max, kwenye orodha ya washua nitoe😂🤣
 
Story za JF sio za kuzichukulia serious, humu kila mtu anapiga goli 5, kila mtu ana mwanamke mkali, kila mtu anamiliki gari, kila mtu ana nyumba kali, kila mtu ana degree na amesoma UDSM, kila mtu alipata division 1 form 4 na six na ana GPA kali.
Hapo kwenye kupiga goli😁🤣mbona Inawezekana Ila mbona mimi Sina gari, Sina mke mkali, Sina nyumba wala kiwanja

Nina leseni tu ya udreva na degree yangu plus jobless Intelligent businessman hatuna maisha tutoe kwenye hilo kundi
 
Back
Top Bottom