Hii tabia ya uvutaji wa sigara ovyo ikomeshwe

Hii tabia ya uvutaji wa sigara ovyo ikomeshwe

Hii kiafya ni hatari kwakweli kama sio kushangaza basi inasikitisha yaani wizara husika hazijishughulishi kabisa...

Viongozi wengi wa hii nchi wako katika comfort zone ndio maana karibia kila kitu wananchi tunawashtua ndio wao wanakurupuka na kukitekeleza.

Kama wanavyoipromote chanjo basi na huu uvutaji hovyo wa sigara wauvalie njuga la sivyo upambanaji wa UVIKO19 utakua hauna maana kama tunaacha magonjwa kama kifua kikuu.

Hili tatizo kwa viongozi hawawezi kuliona kilahisi, ila sisi wazee wa informal sector/sekta zisizorasmi tunakeleka na kuteseka sana maeneo tunayofanyia kazi.

Tamko la serikali lina nguvu kwahiyo wafanye jambo hapa.

hata mabago yarudishe kwenye makutano ya umma
Hivi hakuna kiongozi wa ngazi za juu kwenye utawala huu anayevuta fegi,??
 
ndio maana mimi huwa nawavizia wakisha fika mbalinawatandika mawe mafaka hao [emoji1787][emoji2223]
 
Sigara ni moshi wa mimea ambao hata ukichoma nyasi tu madhara yanafanana. Vipi magari yanayochoma diesel, petrol na viwanda vinavyunguza maplastic mshaviondoa katikati ya makazi. Inahitaji miaka mitano kwa mvuta sigara mmoja kutema kilo moja ya hewa ukaa ila hilo lori lako la taka hutema zaidi ya kilo 50 za hewa ukaa kwa siku na mnapishana nalo kila siku
 
Ni ujinga kwanini wasifanye kisiri?mbona wavuta bange wanajichimbia chimbo ,huu ujinga upo hapa kwetu ,ulaya kwenye vyuo ,hospital na sehemu zenye mikusanyiko kunakuwa na sehemu special ya kuvuta sigara,hata kama kwetu hamna hizo sehemu siyo mtu anawakuta sehemu huku anavuta
 
Na wewe zitakuwa hazikutoshi! Kama umekutana na hiyo kadhia unatakiwa kuchepuka njia au kurudi nyuma ulikotoka ili ujiokoe na huo Moshi! Kulazimisha kuongozana naye umeyataka hivyo vumilia na ikikupendeza gongoe arifu mwende sawa! Tuache tuvute Kwa raha zenu Kama ninyi mnavyojisikia raha mnapokunywa al- kasus!
Tuchepuke njia gani ikiwa kila njia unayopita unakutana na wavuta sigara. Wewe inakuathiri vipi wengine wakinywa alkasus?
 
Sigara ni moshi wa mimea ambao hata ukichoma nyasi tu madhara yanafanana. Vipi magari yanayochoma diesel, petrol na viwanda vinavyunguza maplastic mshaviondoa katikati ya makazi. Inahitaji miaka mitano kwa mvuta sigara mmoja kutema kilo moja ya hewa ukaa ila hilo lori lako la taka hutema zaidi ya kilo 50 za hewa ukaa kwa siku na mnapishana nalo kila siku
Ndo mana kuna sera mbalimbali kikawaida hata viwanda havipaswi kujengwa kwenye makazi ya watu vilevile matumizi ya magari yana muda maalumu ya kutumika au kuwe na mbadala wa nishati zaidi ya hapo na yenyewe ni uchafuzi vilevile.
Sigara licha ya uchafu pia inaleta kero ya harufu.
 
Back
Top Bottom