Hii tabia ya Wanamichezo kumsifia Rais wa nchi kwenye kila jambo tuiitaje?

Ngoja tugungwe tumsifie vizuri
Umeniwahi Mkuu na Mimi kutokana no huu Upuuzi wa hawa Mashabiki wa Vilabu vya Simba na Yanga Kumsifia zaidi Rais Samia badala ya Vilabu vyao / Timu zao naziombea ZIFUNGWE zote hapa hapa Tanzania Ijumaa na Al Ahly na Jumamosi na Mamelodi Sundowns FC.

Inakera sana na Kuboa mno tu Mkuu.
 
Ile ya mabango ya rais naona wamejishtukia baada ya kuripoti sana sasa hivi wameacha.
 
Kwanza kabisa niseme mama anaupiga mwingi, juhudi zote hizi ni kutokana na jitahada za mama... Haya lete hoja yako sasa
 
Post #2 tu inaonyesha upumbavu wa bàadhi ya Watanzania. Wala usidhani ni ugonjwa, ni uvivu tu wa kufikiri uliopelekea bàadhi ya wajinga kudhani ukimsifia Rais hata Kwa yasiyomhusu utaonekana na kutafutiwa nafasi Fulani. Wengine ni vihela vya vocha tu vinawatoa fahamu.
Timu ya riadha imeenda all African games imerudi patupu haikupokelewa hata na Mtendaji wa Kata ya Kimbiji. Wanasiasa wanataka ku-engage na watu waliofanikiwa tayari.
 
Namshukuru Mama Samia, Leo mvua imenyesha kidogo, hii ni dalili ya ushindi kwa Timu yangu hapo kesho
 
Kuna vitu ambavyo Rais Samia yeye mwenyewe kwa mawazo yake au washauri wake wa karibu ameweza kusaidia kwakiasi fulani kwenye michezo hasa soka.

Ukiacha kuchangia fedha kwa kila goli katika hatua fulani za mashindano ya soka , amejaribu kuhamasisha soka, na safari hii ata katika michezo ya jumuia ya madola tumepeleka wachezaji kiasi japo si kwa michezo yote.

Kikubwa uhusiano wa serikali na chama cha mpira umekua mkubwa Sana kuliko awamu zote za uongozi.

Soka limefaidika zaidi kuliko michezo yote
Kama kuna haja ya kusifiwa aendelee kusifiwa kwakua hakuna ubaya wowote kumsifia wakati kuna vitu ameufanyia mpira wetu, na hata asingefanya hakuna mtu angeweza ku muuliza.

Kama kusifiwa kwake wewe inakuuma basi ao watoaji wa sifa wange ambatanisha na kipande Cha kukusifu nawe pia ndugu popoma.
 
Unyumbu ni Tabia ya watu kuahirisha kufikiri kwasababu ya kujipendekeza ,uoga, wa viongozi Wao ama kutumikia kundi fulani kwa masirahi binafsi
 
Ile ya mabango ya rais naona wamejishtukia baada ya kuripoti sana sasa hivi wameacha.
Tegemea kuyaona upya tena Kesho Ijumaa na Keshokutwa Jumamosi sawa Mkuu?
 
Kuna zile zama tulisifia kupatwa kwa Jua kuwa kuliletwa na Mkuu Kaya.

Usiwe na shaka Mkuu ni zama tu zinapita.
Huyu Popoma mwenyewe kipindi kile na yeye alikua hata akijamba anamsifia mwendazake, nashangaa leo hii roho inamuuma mama akisifiwa na chawa wake.
Kwa akili hizi za kusifu na kuabudu viongozi tulizonazo waafrika hata tupewe miaka 1000 mbele bado Afrika yetu itabaki vile vilevile ya kuomba misaada ya kujengewa vyoo na wahisani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…