fasiliteta
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 2,372
- 4,090
Ni wazi kwa sasa Tanzania imeungana na nchi nyingine katika kufata taratibu zinazoitwa za kuzuia maambukizi ya mlipuko wa corona wimbi la tatu katika jamii.
Imekua ni week iliyoanza kwa tahadhari na inaendea kuisha ya matamko ya wimbi la tatu ya Janga hili la Covid-19 kuanzia kwa madaktari na mpaka viongozi wa serikali.
Tatzo si hayo matamko ila sasa naona kama tunafanya usanii. Tahadhari muhimu sizioni zaidi ya maigizo tu. Kama Ni maigizo kwa ajili kupata vimkopo na sisi kama wanavyotaka IMF basi hebu tuongeze kidogo degree ya huu usanii unaoendelea mpaka maana haiwezekani watu masokoni wamejazana vibaya mno hasa kuanzia KKOO, Ilala, Manzese, Mbagala, Tandika, na masoko mengine.
Mechi za mpira uwanjani kama kawa ni nyomi la kufa mtu huku tukisubiri tarehe 03/07 kwa ajili ya mechi iliyoahirishwa ya watani wa jadi ambayo uwanja unatarajiwa kuktapika zaidi.
Hebu tuangalie hata usafiri wetu wa mwendokasi jinsi unavyojaza mpaka watu kupumuliana na kupakazana jasho tupu na mafoleni haya.
Daladala ndo usiseme kabisaa Maana watu ni kama wanakumbatiana na kuhemeana mdomoni
Hata hao viongozi ni usanii tu maana kuna mikutano wanaenda wakiwa na mibarakoa tele lakini mingine hakuna hata barakoa wala tahadhari, hebu waangalie MaDC wakati wanaapishwa na kukabiziana ofisi yani no barakoa no tahadhari, tunamdanganya nani?
Tumekataaa na kupingana na mbinu alizoziasisi JPM lakini hizo za ki-science tunazozitaka tunashindwa kabisaaa kuziendea.
Lastly niseme tu acheni usaniiiii na kuwatia watu hofu kwa matamko lukuki huku hamchukui tahadhari za maana kama mnavyoona nchi za wenzetu hata majirani Kenya na Uganda.
Kwako mama SSH, umejiandaaje na hilo mnalosema wimbi la tatu la Covid-19? Je umekagua Hospital zako vizuri? Zinatosha vifaa tiba?
Una wataalamu wa afya wa kutosha? Vp chakula kinawatosha wananchi? Mmejipangaje?
Je, mmetoa awareness kwa wataalamu wa afya? Maana mwaka Jana kila ukienda hospital ikatokea umekohoa kidogo tu, wauguzi wanakunyanyapaa sanaaa mpaka wagonjwa wakaamua kutoroka na kurudi kujiuguza majumbani kuepuka unyanyapaa zaidi.
Ushauri wangu level seat kwenye usafiri wa umma ni muhimu kuzingatiwa zaidi na tena iwe jambo endelevu na si kwa ajili ya corona tu.
Mwendokasi waache kufanya biashara na watoe huduma sasa,inachosha wanavyofungia magari ili watu wajazane na kubanana mpaka kukosa pumzi.
Ahsante