Hii tamu lakini ni chungu pia

Hii tamu lakini ni chungu pia

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Unapotaja Wachezaj Ambao Waliweza Kucheza Soka Ktka Kiwango Bora Ktka ULimwengu Wa Soka Katka Nafasi Za Kiungo Utawataja, Lothar Mathaus Ambay Inaaminika Ni Kiungo Bora Mzuiaji Kuwah Kutokea, Utamtaja Zinedine Zidane Ambay Sina Haja Ya Kumuelezea, Huwez Msahau Andres Iniesta, Fernando Redondo Na PauL Scholes Lakin Katka Hawa Wote Ni Zidane Pekee Ambay Ameweza kujarib Kuwa Kocha na Kupata Mafanikio Ktka ULimwengu mwingine Tofaut Na Uchezaj, Je Wengine Wapo Wapi Na Wanafanya Nin??

Ktka Wataalam Hawa Ambao Siku Zote Ni Watu Muhim Kwenye Timu, Ni PauL Scholes Na Zizou Ndio Ambao Wamejarib Kurud Tena Kwenye UKimwengu Wa Soka Kama Makocha Huku Zizou Akipata Mafanikio Na Scholes Akishindwa Kufanikiwa Akiwa Kama Kocha. lakin Cha Kushangaza Zaid Ni Kwamba Watu Kuamin Unaposhindwa Kufanya Jambo Wew Basi Huruhusiwi Kutolea Maelezo Yoyote Kuhusu Jambo LiLe Kitu Ambacho Si Sahihi.

Miaka Michache ILiyopita PauL Scholes Alisema Kuwa Ligi Ya Uingereza Inaonekana Ina Ushindan Na Bora Kwa Sababu Timu Nyingi Hazitofautian Sana Ktka Ubora Na Hiyo Inafanya Kuwa na Ushindan Pale Zinapokutana Timu MbiLi Hata Zikiwa Ni Ya Kwanza Na Ya Mwisho Basi Sio Game Za Kutabirika Kwa Sababu Ubora Wa Timu Hizi Haupishan Sana Zaid Ya Timu Moja Kuwa Ba Bajeti Kubwa Na Wachezaj Wachache Wanaoweza Kuamua Mechi.

Wachambuzi Wengi Waliipinga KauLi Hii Wakiamin Kwamba Jamaa Amekuwa Na Dharau na Tangu Amestaafu Yey na Alipoondoka SAF Basi Kwenye Ligi Ya Uingereza Hakuna Ubora Wowote ULioweza Kujidhihirisha Kutoka Kwenye Ligi Hii Lakin Binafsi Nikwambie Ukwel Ni Kwamba Maneno Haya Ya Paul Scholes YaLikuwa na Ukwel Ndani Yake Sema Ndiyo ULikuwa Ukwel Mchungu WaswahiLi Wanaweza Kukwambia *Tamu Lakin Chungu*.

UkiangaLia Maneno Haya Ya Scholes Ambayo Alifanya Comparison Na Laliga Alisema Kabisaa, Ukiwaangalia Madrid, Barca Na Atletico Madrid Za Kuanzia Miaka Ya 2011 ZiLikuwa Timu Hasa Zikichochewa Mafanikio Yao Kama Wapinzan Na Kama chachu Ya Mafanikio Na HiLi Lilifanya Timu Hizi Kuwa Bora Kiasi Kwamba Kuonyesha Timu Nyingine Hazina Upinzan Kabisaa Kwao Na Kuondoa Ubora Wa Ligi Na Watu Kutovutiwa Na Kutazama Mechi Kwa Sababu Ya Mechi Nyingi Kuwa Na Matokeo Ya Kutabirika. Ubora Wa Madrid, Barca Na Atletico ULifanya Ligi Kuea Ya Timu Chache Na Kufanya Watu Wengi Kuamin Ligi Haina Ubora Kwa Sababu Ya Kuwa Na Timu Dhaifu Lakin Uhalisia Ni Kwamba Madrid, Barca Na Atletico Madrid Walikuwa Bora Sana KuLiko Wengine Na Kufanya Ushindani Upotee Kwenye Ligi.

Lakin Baada Ya Pep Guardiola Kuondoka, Atletico Madrid Kupoteza Identity Yake Kutoka Kwenye Defensive Game Yao Na Madrid Kuondokewa Na Zidane Na Ronaldo Kwa Pamoja, Huku Messi Akiibena Barca Wakat Akielekea Uzeen, Ubora Wa Timu Hizi Umeshuka Na Kutokuwa ULe Wa Miaka Michache ILiyopita Na Hatimaye Sasa KiLe Alichokuwa Anasema Scholes Kimejidhihirisha Tena Kutoka EPL Kwenda La Liga Kwa Maana Sasa Laliga Inaonekana Ina Ushindan Zaid Ukiangalia Game Na Msimamo Wa Ligi Na Siku Hizi Mhindi Amekuwa Anapata Faida Zaid Kupitia Vilabu Vya Madrid Na Barca

Lakin Hali Imekuwa Tofaut Kidogo Pale EPL Kwa Maana KiLe KiLichokuwa Kinatokea La Liga Ndiyo Kimehamia Pale Kwa Misim Mi3 MfuLuLizo Huku City na Liverpool Wakiwa Ktka Ubora Wa Juu Sana Na Wengine Wakibaki Kama Wasindikizaj. Pep GuardioLa Amekuwa Akiweka Utawala Wake Kupitia Aina Ya Soka Wanalocheza Huku Jurgen Klopp Yey Anaamin Zaid Katka Mfumo Wa Soka La Gegen Pressing Ambalo Ni Aina Ya Soka La Tofaut Kabisaa Na LiLe La Guardiola Lakin Limekuwa Na Matokeo Chanya Popote Pale Ambapo Jurgen Klopp Amekuwa Anakaa Kwa Muda Mrefu. Ubora Wa LiverpooL Na City Na Kuporomoka Vibaya Kwa Man Utd, Arsenal Na Chelsea Kumefanya Ligi Ya Uingereza Kuwa Ligi Ya Timu MbiLi Huku Hata Wale Wa chini Wakiweza Kuwazuia Hawa Walioporomoka Lakin Wakikosa La Kufanya mbele Ya City Na LiverpooL Na Hapo Ndipo Maneno Ya Scholes Yanaporud Tena Kwenye Ubira Na Kusema Kwamba Ubora Wa City Na LiverpooL Ni Mkubwa Sana Na Ndiyo Unafanya Ligi Kuwa Mbio Za Timu MbiLi Japokuwa Leicester Na Chelsea Hawapo Mbali ILa Gap Alilotengeneza Liver Linaonyesha Kwamba Si Kwa Sababu Ligi Ni Dhaifu ILa Ni Kwa Sababu Wao Ni Bora Sana KuLiko Timu Nyingine.

Ubora Wa Hizi Wa Timu Ni Mara Chache Sana Una Impact Kwa Champions League Kwa Maana KuLe Ni Mbinu Za Makocha Na Bahat Zimekuwa Zinaplay Part Kubwa Sana Kwenye Matokeo KuLiko Ubora Wa Timu Pekee.

Ni kawaida Kwa Ubora Wa Kitu Chochote Kupungua Pale Inapofika Kwenye Peak Level Yake Na Ndivyo ILivyokuwa Kwa Madrid, Barca Atletico Na Bayern Na Sasa Ni Liver Ndio WanakimbiLia KiLeleni Cha Msingi Wakat Huu Ni Kwamba Unapokuwa Juu Tumia Wakat Huu Kufikia Malengo Yote Unayotaka Kuyafikia Na Haya TuLiyaona Kwa City, Madrid, Barca, Bayern BiLa Kuwasahau Dortmund Na Liver Wakiwa Wameanza Na UCL Naamin Watafikia Malengo Yao Makuu Ambayo Ni Kubeba Ubingwa Wa Ligi ya Uingereza Kombe Wanalomiss Kwa 20 Sasa Na ILi LiverpooL Waendelee Kuwa Juu Hawatakiwi Kuridhika na Hiki Ndicho Kinawasukuma Zaid Kwa Sasa Wafanye Hiki Wanachofanya na Waendelee Kuwa Bora

Nimalizie Kwa Kuwakumbusha Tu Kwa Mara Nyingine Ni Kwamba Inawezekana Watu Wanaamin Ligi Ya Uingereza Imepoteza Ubora Miaka Ya Karibun Lakin Ukwel Ni Kwamba City na LiverpooL Wamekuwa Kwenye Ubora Mkubwa Sana Na Wataendelea Kuwa Hivi Mpaka Wengine Watapoamua Kujiimarisha Au Wao Watapokumbwa Na Anguko Ambalo Ni Mzunnguko Wa Kawaida Kwa Pale Unapokuwa Juu Kwa Muda Mrefu

IMG-20200106-WA0100.jpeg
IMG-20200106-WA0097.jpeg
IMG-20200106-WA0085.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom