Hii Tanzania una shida gani? Niko mbioni kubadilisha kuwa Raia wa canada

Hii Tanzania una shida gani? Niko mbioni kubadilisha kuwa Raia wa canada

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
WASAIDIZI WA RAIS WAJITATHIMINI HARAKA.

Na Thadei Ole Mushi.

Rais Samia anawezekana anaitakia hii nchi Mema sana ila wanaomzunguka na washauri wake haswa wa Uchumi wakamwangusha.

BOT wameweka limit na masharti kibao kuhusu watu kutoa fedha za Kugeni kwenye Account zao. Tafsiri yake ni kwamba akiba ya fedha za Kigeni imepungua sana. Kama hali itaendelea hivi Muda si Mrefu tutashindwa kuagiza mafuta kwa kuwa hatuna fedha za kuagizia matokeo yake kutakuwa na ongezeko la Mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na baadhi ya Shughuli za kiuchumi kuzidi kudorora.

BOT wao wameona Solution ni kuzuia fedha za watu zisitoke ili kunusuru hali ya Mambo. Hawa ndio washauri wakuu wa Rais kuhusu Uchumi…. Sijui ila naona kuna tatizo sijasoma uchumi ila hata kwa darasa la Saba B anaweza kuona hili.

Tutapataje fedha za kigeni kama;-

Tunaimport toothpics
Tunaimport Mchele
Tunaimport Sukari
Tunaimport Ngano
Tunaimport chuma
Tunaimport Samaki
Tunaimport mafuta ya Kula
Tunaimport Maziwa ya Unga

Tunavyozungumza sasa hivi hapo mpakani kati ya Kenya na Tanzania Mahindi wamezuiwa yasitoke nje ya nchi. Wafanyabiashara wanalia kuwa mahindi yao yanaharibika kwa kuwa mengine ni mabichi…..

Leo waziri (Jafo) anafungia Bar zinazoleta Kelele mtaani kesho Mkuu wa Mkoa anafungulia tena kwa Kejeli kabisa utafikiri ni Serikali Mbili tofauti hawa viongozi wanatokea.

Sasa hivi solution ya kila tatizo Tanzania wananchi wameamua kulitatua kwa njia ya Mgomo. Migomo na maandamano vinazidi kushamiri katika kila tatizo. Tafsiri yake ni kuwa Mfumo unataka ku- Collapse….

Nadharia za Fizikia hazidanganyi wanasema “ Ukiweka karibu sana kitu na jicho lako hutakiona vizuri” jaribu kuweka kidole chako karibu sana na Jicho lako hutokiona vizuri. Ukitaka kukiona vizuri kisogeze Mbali. Mhimili umepata ugonjwa unaoitwa “hyperopia” kutokuwa na uwezo wa kuona vitu vilivyopo karibu.

Tanzania ya Watu Milioni 60 plus tukijitafuta humo ndani tunaweza kutoka tulipo. Rais ana nia njema sana na Taifa hili tatizo kubwa naliona kwa watu waliopewa jukumu la Kumsaidia wapo karibu sana na mfumo hivyo ni ngumu kuona hata pale wanapokosea.
 

Attachments

  • FB_IMG_1685705404355.jpg
    FB_IMG_1685705404355.jpg
    81 KB · Views: 5
Upo kama mimi, niko mbioni kuomba uraia wa nchi hizi

Angola
Namibia
Bostwana

Nazipenda hizi nchi, nikipata uraia huo nahamisha na familia yangu na kuanza mizizi yangu huko
 
Upo kama mimi, niko mbioni kuomba uraia wa nchi hizi

Angola
Namibia
Bostwana

Nazipenda hizi nchi, nikipata uraia huo nahamisha na familia yangu na kuanza mizizi yangu huko
Mimi niko mbioni kuomba uraia

Haiti
Central Africa Republic
Bangladesh

Hivi Gilbert A Massawe anafanya kazi BOT.

R.I.P Thadei
 
Back
Top Bottom