pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,913
- 13,876
Ikiwa yamebaki masaa machache kabla ya mechi ya marudiano na club Africain pale Tunis, TFF imetoa taarifa ya matukio ya mechi zilizopita baada ya kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya NBC kutoa maamuzi ya matukio ya mechi zilizopita.
Huku baadhi ya wachezaji na waamuzi kupewa adhabu, huku Chama na Ki Aziz kupewa adhabu ya mechi tatu kwa kila mmoja na faini ya laki tano kila mmoja. Hiyo ni kawaida, ila kilichonishangaza ni baadhi ya mashabiki wa Dar es Salam Young Africans kuwemo kwenye adhabu hiyo.
Kamati hiyo imewafungia mashabiki na wanachama wanne wa Yanga miezi mitatu kwa kosa la kuwavamia waamuzi wa mchezo kati ya Simba na Yanga wakati wa mapumziko kabla walinzi wa uwanjani (stewards) hawajaamua ugomvi huo.
Mashabiki na wanachama wa Dar es Salam Young Africans walionekana wakifanya tukio hilo kupitia camera za CCTV zilizopo eneo hilo wakiwa wanaelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Wakati mashabiki wakikumbana na adhabu hiyo na klabu yao imepigwa faini ya million tano (5,000,000/=), baada ya kuingia uwanjani kupitia mlango usio rasmi wakati wa mchezo wao dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya moja moja.
Kumbuka hiyo siyo mara ya kwanza kupitia mlango usio rasmi, hiyo ni kawaida yao hata mechi iliyopita waliacha basi lao kubwa na kuja na coaster mapaka uwanjani. Huku basi likiwa na dereva tu na wakapita mlango usiyo rasmi walipewa onyo, safari hii wamerudia tena wamepigwa rungu la million tano.
Yaani hawa jamaa ndiyo maana wakienda kule CAF Champions League hawadumu, maana wao wanaendekeza ushirikina na kuwarubuni waamuzi wa mchezo husika ili awe upande wao, kumbe mpaka mashabiki wao ni vigagula!
Wakati huo Club Africain wamepeleka malalamishi CAF kwa kile walichofanyiwa pale Benjamin William Mkapa Stadium. Huko nako hawatatoka salama, watakula tena faini wakati huo hawana manufaa yoyote waliyopata. Sisi tulivyowasha moto pale kwa Madiba ulitusaidia, maana ilikuwa kuna baridi. Sasa estadio de utopolo wanafanya mambo kienyeji sana tena bila manufaa.
NB: Badala mroge kimataifa mpate hela mnaroga mechi ya derby. ambayo mwisho wa msimu mshindi millioni 100. Kweli kupanga ni kuchagua!