Hii timu kweli inahitaji msaada

Hii timu kweli inahitaji msaada

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Ikiwa yamebaki masaa machache kabla ya mechi ya marudiano na club Africain pale Tunis, TFF imetoa taarifa ya matukio ya mechi zilizopita baada ya kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya NBC kutoa maamuzi ya matukio ya mechi zilizopita.

Huku baadhi ya wachezaji na waamuzi kupewa adhabu, huku Chama na Ki Aziz kupewa adhabu ya mechi tatu kwa kila mmoja na faini ya laki tano kila mmoja. Hiyo ni kawaida, ila kilichonishangaza ni baadhi ya mashabiki wa Dar es Salam Young Africans kuwemo kwenye adhabu hiyo.

Kamati hiyo imewafungia mashabiki na wanachama wanne wa Yanga miezi mitatu kwa kosa la kuwavamia waamuzi wa mchezo kati ya Simba na Yanga wakati wa mapumziko kabla walinzi wa uwanjani (stewards) hawajaamua ugomvi huo.

Mashabiki na wanachama wa Dar es Salam Young Africans walionekana wakifanya tukio hilo kupitia camera za CCTV zilizopo eneo hilo wakiwa wanaelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Wakati mashabiki wakikumbana na adhabu hiyo na klabu yao imepigwa faini ya million tano (5,000,000/=), baada ya kuingia uwanjani kupitia mlango usio rasmi wakati wa mchezo wao dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya moja moja.

Kumbuka hiyo siyo mara ya kwanza kupitia mlango usio rasmi, hiyo ni kawaida yao hata mechi iliyopita waliacha basi lao kubwa na kuja na coaster mapaka uwanjani. Huku basi likiwa na dereva tu na wakapita mlango usiyo rasmi walipewa onyo, safari hii wamerudia tena wamepigwa rungu la million tano.

Yaani hawa jamaa ndiyo maana wakienda kule CAF Champions League hawadumu, maana wao wanaendekeza ushirikina na kuwarubuni waamuzi wa mchezo husika ili awe upande wao, kumbe mpaka mashabiki wao ni vigagula!

Wakati huo Club Africain wamepeleka malalamishi CAF kwa kile walichofanyiwa pale Benjamin William Mkapa Stadium. Huko nako hawatatoka salama, watakula tena faini wakati huo hawana manufaa yoyote waliyopata. Sisi tulivyowasha moto pale kwa Madiba ulitusaidia, maana ilikuwa kuna baridi. Sasa estadio de utopolo wanafanya mambo kienyeji sana tena bila manufaa.

NB: Badala mroge kimataifa mpate hela mnaroga mechi ya derby. ambayo mwisho wa msimu mshindi millioni 100. Kweli kupanga ni kuchagua!
 
Kama unatumia akili kamili ,jibu maswali yafuatayo.

1. Ile mechi iliyofungwa na Azam , yanga alihongwa refa?

2. Mechi uliyosuluhu kwa mbinde na kmc yanga ilihonga?

3. Goli mlilowafunga prison,nje ya nyavu na lilikubaliwa,yanga alihongwa?

4, Huko CAF tutajie kombe lolote ulilowahi kuchukua ili tuige mafanikio yako.

5. Rushwa ya kumuhonga shabani kado wa mtibwa, kabwili wa yanga iliishia wapi.

6, Ukiondoa makundi ya walemavu, Ni kombe gani ambalo unalo ,litaje na uonyeshe.
 
Tuendelee au tuishie apa?

Screenshot_20221108-203519.jpg
 
Jichanganye nije na video zikiwahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa Simba wakifanya Ulozi live.
 
Kama unatumia akili kamili ,jibu maswali yafuatayo.

1. Ile mechi iliyofungwa na Azam , yanga alihongwa refa?

2. Mechi uliyosuluhu kwa mbinde na kmc yanga ilihonga?

3. Goli mlilowafunga prison,nje ya nyavu na lilikubaliwa,yanga alihongwa?

4, Huko CAF tutajie kombe lolote ulilowahi kuchukua ili tuige mafanikio yako.

5. Rushwa ya kumuhonga shabani kado wa mtibwa, kabwili wa yanga iliishia wapi.

6, Ukiondoa makundi ya walemavu, Ni kombe gani ambalo unalo ,litaje na uonyeshe.
Mimi Yanga mwenzio. Ila hapa naungana na Hersi...wewe mla mihogo. Simba Kimataifa ipo nafasi ya juu si kama sisi. Tuache tu Upumbavu. Kuna mambo tuache kutiana Ujinga. Angalia kwenye Ranks za CAF na FIFA sisi tupo wapi na wao wapo wapi. Si wakati wote wa kuleta ushabiki choo. Tukubali ukweli.
 
Wewe kweli kilaza. Kwa hiyo kufanikiwa lazima uchukue kombe? Tanzania ikifuzu kushiriki world cup haitakuwa imefanikiwa kwa level fulani mpaka ichukue kombe?
 
Hakuna timu iliyowahi kubeba kombe la vilabu vya Africa Kwa kutumia hongo Kwa waamuzi na uchawi.
Uchawi mbaka mnapigwa fine, mambo ya aibu alafu mnaita mafanikio.
Wekezeni kwenye utaaalamu sio chupri.
 
Kwa hyo yale maji ya maiti mliyo wamwagia club africain kwenye mechi iliyopita yalikuwa ya kuogea yale subirini rungu la Caf
 
Mimi Yanga mwenzio. Ila hapa naungana na Hersi...wewe mla mihogo. Simba Kimataifa ipo nafasi ya juu si kama sisi. Tuache tu Upumbavu. Kuna mambo tuache kutiana Ujinga. Angalia kwenye Ranks za CAF na FIFA sisi tupo wapi na wao wapo wapi. Si wakati wote wa kuleta ushabiki choo. Tukubali ukweli.
Na thamani na hisa za club inapanda au kushuka kutokana na position hzo za Caf champions league na FIFA haijalisha umechukua kombe au la ila ukifika hatua nzuri kimataifa inakuwa hvyo sasa hao manara kashawakamata masikio hakuna wanachofikiri zaid ya kushangilia unbeaten ya mchongo
 
Ikiwa yamebaki masaa machache kabla ya mechi ya marudiano na club Africain pale Tunis, TFF imetoa taarifa ya matukio ya mechi zilizopita baada ya kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya NBC kutoa maamuzi ya matukio ya mechi zilizopita.

Huku baadhi ya wachezaji na waamuzi kupewa adhabu, huku Chama na Ki Aziz kupewa adhabu ya mechi tatu kwa kila mmoja na faini ya laki tano kila mmoja. Hiyo ni kawaida, ila kilichonishangaza ni baadhi ya mashabiki wa Dar es Salam Young Africans kuwemo kwenye adhabu hiyo.

Kamati hiyo imewafungia mashabiki na wanachama wanne wa Yanga miezi mitatu kwa kosa la kuwavamia waamuzi wa mchezo kati ya Simba na Yanga wakati wa mapumziko kabla walinzi wa uwanjani (stewards) hawajaamua ugomvi huo.

Mashabiki na wanachama wa Dar es Salam Young Africans walionekana wakifanya tukio hilo kupitia camera za CCTV zilizopo eneo hilo wakiwa wanaelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Wakati mashabiki wakikumbana na adhabu hiyo na klabu yao imepigwa faini ya million tano (5,000,000/=), baada ya kuingia uwanjani kupitia mlango usio rasmi wakati wa mchezo wao dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya moja moja.

Kumbuka hiyo siyo mara ya kwanza kupitia mlango usio rasmi, hiyo ni kawaida yao hata mechi iliyopita waliacha basi lao kubwa na kuja na coaster mapaka uwanjani. Huku basi likiwa na dereva tu na wakapita mlango usiyo rasmi walipewa onyo, safari hii wamerudia tena wamepigwa rungu la million tano.

Yaani hawa jamaa ndiyo maana wakienda kule CAF Champions League hawadumu, maana wao wanaendekeza ushirikina na kuwarubuni waamuzi wa mchezo husika ili awe upande wao, kumbe mpaka mashabiki wao ni vigagula!

Wakati huo Club Africain wamepeleka malalamishi CAF kwa kile walichofanyiwa pale Benjamin William Mkapa Stadium. Huko nako hawatatoka salama, watakula tena faini wakati huo hawana manufaa yoyote waliyopata. Sisi tulivyowasha moto pale kwa Madiba ulitusaidia, maana ilikuwa kuna baridi. Sasa estadio de utopolo wanafanya mambo kienyeji sana tena bila manufaa.

NB: Badala mroge kimataifa mpate hela mnaroga mechi ya derby. ambayo mwisho wa msimu mshindi millioni 100. Kweli kupanga ni kuchagua!
Sawa kigagula🦁🤸
 
Back
Top Bottom