Hii 'tumbua teua' sio gharama kwa Nchi? Kama sio mbona Mkuchika na Ndumbaro hamfanyi hivyo?

Tila-lila2

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
652
Reaction score
1,058
Rais wangu hujali gharama, anatoka mtu unaweka mtu. Hata kama katoka ncha nyingine ya nchi hujali gharama za kumhamisha. Unawapa ulaji. Hasa wale watumishi wa umma wenye elements za kiCCM. Safi sana!

Aliyechukua nafasi ya Katambi wa Dodoma anatoka Geita, anakuja kulipwa mahela na maslahi mengine ya Ukuu wa Wilaya - kwa muda mfupi tu. Hukutaka nafasi ya Katambi mtu wa Ofisini kwake au hata wa Mkoa wa Dodoma akaimu. Umemtoa - na yeye pia atalipwa mahela na yatamsaidia kwenye Kampeni zake za kuwania Shinyanga Mjini.

Safi sana Rais wangu, hujali gharama - mtu anatoka na mahela yake unamweka mwingine na kumpa mahela yake. Wote hao kina Ole Sendeka, Mkenda na wote hao, wanaondoka na neema unawaleta wengine kwenye neema!

Sasa huku kwa wanaosimamiwa na kina Mkuchika hali sio hivyo Rais wangu. Hali ni mbaya sana. Watu wanakaimishwa miaka zaidi ya miwili. Utumishi wamekalia tu barua za kuidhinisha watumishi kwenye nafasi zao. Mtu hamna hata shaka kuwa anakaimu nafasi ambayo haina mtu lakini mtu hathibitishwi eti kisa kuepuka gharama kuwa kama hamna barua yakuthibitishwa na Utumishi asilipwe.

Halmshauri watu kibao wanakaimu, wameombewa Utumishi na TAMISEMI lakini hawathibitishwi. Mpaka ninaacha utumishi wa Umma Mwaka 2017 nilikuwa nimeshakaimu zaidi ya miaka miwili na nusu. Haki iko wapi Ndumbaro na Mkuchika? Nimewaacha wenzangu wanakaimu na mpaka sasa wanakaimu. Acheni roho mbaya wapeni watumishi wanachostahili walipwe kwa nafasi wanazotumikia.

Angalieni Rais asivyopenda watu kukaimu. Mtu anatoka yeye anaweka mtu substantively. Nyie Utumishi hivi hizo fedha ni za kwenu au za Serikali? Acheni roho mbaya. Mmeharibu sana utumishi wa umma. Mnasababisha Rais achukiwe bure kumbe tatizo ni ninyi. Kama tatizo lingekuwa ni kwa Rais mbona yeye sasa hakawizi. Acheni mambo yenu hayo. Na mwaka huu kwa kweli mnachangia sana kupunguza kura za CCM. Hovyo kabisa ninyi!
 
Enzi zetu za ajira za Permanent and Pensionable zilishapita. Wakati ule muda wa kupanda cheo kama huna makosa yoyote ya kiutumishi na sifa za kitaaluma unazo ulikuwa unapanda cheo na kurekebishiwa mshahara haraka sana na malimbikizo unalipwa. Kwa sasa haya yoye yanategemea "Personal Whims" za mtu mmoja.

Mwenyezi Mungu wanusuru waja wako walioko kwenye Utumishi wa Serikali!!!
 
Rais wangu hujali gharama, anatoka mtu unaweka mtu. Hata kama katoka ncha nyingine ya nchi hujali gharama za kumhamisha. Unawapa ulaji. Hasa wale watumishi wa umma wenye elements za kiCCM. Safi sana!

Aliyechukua nafasi ya Katambi wa Dodoma anatoka Geita, anakuja kulipwa mahela na maslahi mengine ya Ukuu wa Wilaya - kwa muda mfupi tu. Hukutaka nafasi ya Katambi mtu wa Ofisini kwake au hata wa Mkoa wa Dodoma akaimu. Umemtoa - na yeye pia atalipwa mahela na yatamsaidia kwenye Kampeni zake za kuwania Shinyanga Mjini.

Safi sana Rais wangu, hujali gharama - mtu anatoka na mahela yake unamweka mwingine na kumpa mahela yake. Wote hao kina Ole Sendeka, Mkenda na wote hao, wanaondoka na neema unawaleta wengine kwenye neema!

Sasa huku kwa wanaosimamiwa na kina Mkuchika hali sio hivyo Rais wangu. Hali ni mbaya sana. Watu wanakaimishwa miaka zaidi ya miwili. Utumishi wamekalia tu barua za kuidhinisha watumishi kwenye nafasi zao. Mtu hamna hata shaka kuwa anakaimu nafasi ambayo haina mtu lakini mtu hathibitishwi eti kisa kuepuka gharama kuwa kama hamna barua yakuthibitishwa na Utumishi asilipwe.

Halmshauri watu kibao wanakaimu, wameombewa Utumishi na TAMISEMI lakini hawathibitishwi. Mpaka ninaacha utumishi wa Umma Mwaka 2017 nilikuwa nimeshakaimu zaidi ya miaka miwili na nusu. Haki iko wapi Ndumbaro na Mkuchika? Nimewaacha wenzangu wanakaimu na mpaka sasa wanakaimu. Acheni roho mbaya wapeni watumishi wanachostahili walipwe kwa nafasi wanazotumikia.

Angalieni Rais asivyopenda watu kukaimu. Mtu anatoka yeye anaweka mtu substantively. Nyie Utumishi hivi hizo fedha ni za kwenu au za Serikali? Acheni roho mbaya. Mmeharibu sana utumishi wa umma. Mnasababisha Rais achukiwe bure kumbe tatizo ni ninyi. Kama tatizo lingekuwa ni kwa Rais mbona yeye sasa hakawizi. Acheni mambo yenu hayo. Na mwaka huu kwa kweli mnachangia sana kupunguza kura za CCM. Hovyo kabisa ninyi!
CCM italipuka muda si mrefu.
 
Ni awamu hii tu ndipo tumeona watu ambao hawajawahi kuwa watumishi wa umma wanaibuliwa kutoka kwenye mifuko ya koti na kupewa uDAS, uRAS na uDED. Na wataalamu husika wanayajua haya mambo wameufyata kimya
 
Hovyo hovyo!
 
Wengine kutoka majalalani ndiyo maana wakianza kupata mshahara mzuri na marupurupu wanaanza kutongoza wake za watu
 
Duh... naendelea kusoma comment ili niongeze maarifa
 
Ni awamu hii tu ndipo tumeona watu ambao hawajawahi kuwa watumishi wa umma wanaibuliwa kutoka kwenye mifuko ya koti na kupewa uDAS, uRAS na uDED. Na wataalamu husika wanayajua haya mambo wameufyata kimya
Hata wakikuua maiti yako itashuhudia ukweli huu. Hii ni awamu ya ovyo kuliko awamu zote. DAS toka kijiweni???
 
Back
Top Bottom