POTOSHI Hii video camera inadondoka ni kutoka kombe la dunia au ni mechi gani? Tusaidie kuthibitisha

POTOSHI Hii video camera inadondoka ni kutoka kombe la dunia au ni mechi gani? Tusaidie kuthibitisha

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha



1782036556937.png
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni ikidai kuwa kamera ya angani (aerial camera) iliyoanguka uwanjani ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili Kombe la Dunia la FIFA 2026, huku baadhi ya watumiaji wakidai kuwa tukio hilo limetokea katika moja ya viwanja vinavyotumika kwenye mashindano hayo.

Uhalisia

JamiiCheck imefuatiliaji video hiyo na kubaini kuwa tukio hilo halihusiani na Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Uchunguzi unaonesha kuwa kamera hiyo ilianguka kwenye Uwanja wa Nagyerdei uliopo Debrecen, Hungary, tarehe 9 Juni 2026, wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za taifa za Hungary na Kazakhstan. Kamera hiyo ilianguka wakati mchezo ukiendelea na ilimkosa kwa karibu mpiga picha aliyekuwa pembeni mwa uwanja.

Shirikisho la Soka la Hungary (Hungarian Football Federation) limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku vyombo mbalimbali vya habari nchini humo vikiliripoti.

Aidha, Hungary si miongoni mwa nchi zinazoshiriki kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2026, ambalo linafanyika nchini Canada, Mexico na Marekani. Vilevile, Hungary na Kazakhstan hazikufuzu kushiriki mashindano hayo, wala hazikuhusika katika michezo rasmi ya maandalizi ya Kombe la Dunia.
​
Haikuwa kombe la dunia, n video ya Juni 2026 ilikuwa n mechi ya kirafiki kimataifa nchini Hungary
 
Back
Top Bottom