- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Julai 19, 2026 mechi za kombe la dunia mwaka 2026 zilihitimishwa kwa mchezo wa fainali kati ya Hispania na Argentina ya Lionel Messi ambapo Hispania waliibuka mabingwa baada ya kupata ushindi wa bao moja, na hivyo kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mechi iloyochezwa mjini New Jersey nchini Marekani.
Kabla ya mchezo huo kulikuwapo utani mwingi mtandaoni katika ya mashabiki wa mataifa hayo kuelekea fainali amabapo umekuwa ukifanyika kwa video, picha na kadhalika.
Mfano ilichapishwa video inayoonesha Mbuzi akibeba kitambaa kilichowekwa sehemu unapofikia mwanga wa 'projector' na kuwawezesha watazamaji kuangalia mechi inayoonekana kuwa ni Argentina na Barcelona lakini baadaye inaonekana Hispania.
Je, video hiyo ni halisi?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa video hiyo si halisi bali ni tukio lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI)
Kupitia Google reverse image search JamiiCheck imebaini video iliyochapishwa Instagram na ukurasa unaoitwa realisticaivid ikiwa na nembo ya AIVIDEO.COM na kubainisha kuwa imetengenezwa kwa @aivideodotcomcollabs.
Aidha nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa akili unde zinabainisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia hiyo.