SI KWELI Hii video ya paka juu ya bawa la ndege ni halisi au tunapangwa, na kama ni halisi inawezekanaje?

SI KWELI Hii video ya paka juu ya bawa la ndege ni halisi au tunapangwa, na kama ni halisi inawezekanaje?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Watu wa JamiiCheck kwakweli tunahitaji msaada wenu katika hili, hii video ni halisi au wana wanajaribu kutuchezea, na kama ni kweli inawezekanaje?



1758951690010.png
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinachomuonesha mwanamke akiwa ndani ya ndege akipiga kelele kutokana na tukio la Paka kuwa kwenye bawa la ndege inayoruka angani. Video hiyo imesambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Youtube na Instagram.

Uhalisia wa Video hiyo

JamiiCheck imefuatilia video hiyo na kujirirdhisha kuwa si video halisi.

Video hiyo imetengenezwa na moja ya aina ya Teknolojia ya Akili Unde ya Google ijulikanayo kama Veo ambayo alama (Watermark) yake inaoenekeana chini kulia mwa video hiyo.

Ufuatiliaji kwa kutumia mbinu za kidigitali pia zinabainisha baadhi ya dosari ikiwemo baadhi ya mapungufu kwa mtu anayeonekana akirekodi, rejelea mwanzoni mwa video hiyo ambapo mtu huyo haionekani miwani aliyovaa imejishikiza wapi na simu yake haioneshi mwanga halisi na ule unaonekana.

Aidha paka huyo haonekani kuwa na mshtuko katika tukio hilo huku ukilinganisha na kiwango cha upepo pamoja na mwendokasi wa chombo hicho. Mijongeo ya Paka pia haiendani na na tukio la ndege hiyo kupaa.
Inaweza kuwa halisi au si halisi.

Kwa nini si halisi?

Kiumbe hai yoyote hatakiwi kuwa eneo la mijongeo ya ndege nikimaanisha (Airside). Paka mpaka afike Airside ni process ndefu.

Kuna factors nyingi ambazo si rahisi kwa Paka kufika Airside na kama ikitokea kafika na kaonekana eneo la mijongeo ya ndege basi ndege ambayo inatua (HAITATUA) na kama ina takeoff haitawezekana KURUKA.

Mpaka atolewe kwenye Runway or vicinity ya Airside.

Itoshe kusema kwa upande wangu si halisi kwa sababu za kiusalama na access ya Mnyama ndani ya mijongeo ya ndege.

Utaratibu wa shughuli za ndege (Ground operations) upo complex sana..
 
Hii video imetengenezwa na AI program itwayo VEO3
  • Inamilikiwa na kampuni ya Google
  • Ushahidi.
1. WVeo watermark kwenye video
1758966736793.png

2. Video ina sekunde 8: Kwa sasa VEO 3 ina uwezo wa kutoa video clip za urefu huo.
---
1758966893430.png

AI zingine zenye uwezo wa kutoa video clip zenye ubora ni kama: Seedance ( Inamilikiwa na Black Forest Lab)
---
Watu wa JamiiCheck kwakweli tunahitaji msaada wenu katika hili, hii video ni halisi au wana wanajaribu kutuchezea, na kama ni kweli inawezekanaje?

Inafikirisha sana, najaribu kuitoa kasoro nakosa, zaidi zaidi ni akili tu inagoma, kuwa hii si rahisi.
Lakini video ina uhalisia mkubwa saaana.

"Ngoja kwanza nikusanye mawazo yenu nitakuja kuporomosha yangu baadae.' Hivi ndivyo hujibu wajuaji wa mambo wakikwama...

Hii video ni real, angalia mjongeo wa paka

 
Hii video imetengenezwa na AI program itwayo VEO3
  • Inamilikiwa na kampuni ya Google
  • Ushahidi.
1. WVeo watermark kwenye video
View attachment 3480063
2. Video ina sekunde 8: Kwa sasa VEO 3 ina uwezo wa kutoa video clip za urefu huo.
---
View attachment 3480065
AI zingine zenye uwezo wa kutoa video clip zenye ubora ni kama: Seedance ( Inamilikiwa na Black Forest Lab)
---
Basi ai ilipofikia ni nyoko, kesho ukiona video ya mkeo ana PENZIKA usiamini mpaka ushuhudie laive bila chenga 😄
 
Screenshot_20250927_140126_WhatsApp.jpg

Ukiangalia vizuri utaona hiyo wing inainuka lakini paka bado kakanyaga hewani comfortable
 
Basi ai ilipofikia ni nyoko, kesho ukiona video ya mkeo ana PENZIKA usiamini mpaka ushuhudie laive bila chenga 😄
- Sahihi kabisa.
  • Kuna site kama "dfans" - Ni mirror_copy ya onlyfans ( Notice hizo site zinakutaka uwe above 18+)
  • ila kwa dfans scens zote hutengenezwa na AI.
 
- Sahihi kabisa.
  • Kuna site kama "dfans" - Ni mirror_copy ya onlyfans ( Notice hizo site zinakutaka uwe above 18+)
  • ila kwa dfans scens zote hutengenezwa na AI.
Uko nondo mkuu, nitatembelea, nijionee ya dunia
 
Chuma inaenda zaidi zaidi ya 300 km/hr halafu bado aendelee kuwepo hapo mpaka inapaa.??

Hiyo sio kweli
 
Back
Top Bottom