Watu wa JamiiCheck kwakweli tunahitaji msaada wenu katika hili, hii video ni halisi au wana wanajaribu kutuchezea, na kama ni kweli inawezekanaje?
Your browser is not able to display this video.
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinachomuonesha mwanamke akiwa ndani ya ndege akipiga kelele kutokana na tukio la Paka kuwa kwenye bawa la ndege inayoruka angani. Video hiyo imesambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Youtube na Instagram.
Uhalisia wa Video hiyo
JamiiCheck imefuatilia video hiyo na kujirirdhisha kuwa si video halisi.
Video hiyo imetengenezwa na moja ya aina ya Teknolojia ya Akili Unde ya Google ijulikanayo kama Veo ambayo alama (Watermark) yake inaoenekeana chini kulia mwa video hiyo.
Ufuatiliaji kwa kutumia mbinu za kidigitali pia zinabainisha baadhi ya dosari ikiwemo baadhi ya mapungufu kwa mtu anayeonekana akirekodi, rejelea mwanzoni mwa video hiyo ambapo mtu huyo haionekani miwani aliyovaa imejishikiza wapi na simu yake haioneshi mwanga halisi na ule unaonekana.
Aidha paka huyo haonekani kuwa na mshtuko katika tukio hilo huku ukilinganisha na kiwango cha upepo pamoja na mwendokasi wa chombo hicho. Mijongeo ya Paka pia haiendani na na tukio la ndege hiyo kupaa.
Kiumbe hai yoyote hatakiwi kuwa eneo la mijongeo ya ndege nikimaanisha (Airside). Paka mpaka afike Airside ni process ndefu.
Kuna factors nyingi ambazo si rahisi kwa Paka kufika Airside na kama ikitokea kafika na kaonekana eneo la mijongeo ya ndege basi ndege ambayo inatua (HAITATUA) na kama ina takeoff haitawezekana KURUKA.
Mpaka atolewe kwenye Runway or vicinity ya Airside.
Itoshe kusema kwa upande wangu si halisi kwa sababu za kiusalama na access ya Mnyama ndani ya mijongeo ya ndege.
Utaratibu wa shughuli za ndege (Ground operations) upo complex sana..
1. WVeo watermark kwenye video
2. Video ina sekunde 8: Kwa sasa VEO 3 ina uwezo wa kutoa video clip za urefu huo.
---
AI zingine zenye uwezo wa kutoa video clip zenye ubora ni kama: Seedance ( Inamilikiwa na Black Forest Lab)
---
1. WVeo watermark kwenye video View attachment 3480063
2. Video ina sekunde 8: Kwa sasa VEO 3 ina uwezo wa kutoa video clip za urefu huo.
--- View attachment 3480065
AI zingine zenye uwezo wa kutoa video clip zenye ubora ni kama: Seedance ( Inamilikiwa na Black Forest Lab)
---