SI KWELI Hii Video ya tetemeko inayonyesha jengo likianguka Venezuela

SI KWELI Hii Video ya tetemeko inayonyesha jengo likianguka Venezuela

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo na video ambayo imechapishwa na kusambazwa na baadhi ya vyombo vya habari pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii wakidai kuwa inaonesha madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililoikumba Venezuela, ambalo linadaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,450 pamoja na uharibifu mkubwa wa makazi, miundombinu na mali mbalimbali.

Katika kufuatilia uhalisia wa madai hayo kwa kutumia nyenzo za kidijitali, ikiwemo utafutaji wa picha kwa kutumia mbinu ya reverse image search, imebainika kuwa video hiyo si ya tukio linalodaiwa kutokea nchini Venezuela.

Ufuatiliaji kupitia chombo cha khabari cha ihalas news agency umebainisha kuwa video hiyo ilirekodiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Uturuki mwezi Februari mwaka 2023.

Video hiyo imewahi kuchapishwa na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa kuripoti madhara ya tetemeko hilo, lililosababisha maelfu ya vifo na uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu.

Hadi sasa hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa video hiyo inahusiana na tukio lolote la hivi karibuni nchini Venezuela.
VENEZUELA PG.jpg
 
Nilifuatilia kwa Karibu CNN, Al Jazeera, na BBC kulikuwa na jengo kweli linaanguka na walitoa kuwa kama huwezi kustahimili usiangalie lakini siyo hilo kwa urefu
 
Back
Top Bottom