Elections 2015 Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Elections 2015 Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Huwa nawaza wakati mwingine, machaguo yote ya binadamu yaweza kuwa ya Mungu kweli? The fact that we humans are prone to mistakes, basi inawezekana hata ule usemi unaovuma kuwa "chaguo la wengi ni chaguo la Mungu" waweza kuwa si kweli. Hasa nyakati hizi ambapo principles za kupata "chaguo la Mungu" hazifuatwi. One thing for sure, huyo aliyepangwa na "mungu" ndo atakuwa rais wetu.
 
Kuna wagombea wengine wameshaandaa ambulance kabisaaaa! Wakipigwa chini wasife kirahisi, walau wafie mikononi mwa madaktari
 
Sijawahi hata siku moja kufikiri mtu wako atakuwa rais pamoja na kelele zote!na iwapo atakuwa itabidi watanzania tujichunguze akili zetu.
Ndio maana UKAWA wanamtaka huyu jamaa. Kwani akipitishwa itakuwa rahisi kwao kumchinja na kuiua CCM kabisa
 
Kuna wagombea wengine wameshaandaa ambulance kabisaaaa! Wakipigwa chini wasife kirahisi, walau wafie mikononi mwa madaktari
Masikini mashabiki wao. Maana wenyewe hawana ambulance hivyo watafia vijiweni na vi elfu kumi kumi walivyo kuwa wanapewa
 
Mungu anasingiziwa mengi kweli kweli Duniani na haswa Tanzania,lakini Yote hii ni ulaghai na umbumbu pia!!

Hivi Mungu ndo alipanga Kikwete awe raisi na kuwatumia wakina Lowasa na Rostam Aziz wamtafutie uraisi Kikwete??!!

Mungu ndio Kapangwa Ridhiwani Kikwete awe mbunge wa Chalinze huku Baba akiwa raisi na pia Kikwete,Salma na Ridhiwani na yule mjomba wa Bagamoyo wawe wote wajumbe wa NEC??!!

Mungu ndio alipanga Mgabe awe raisi wa Zimbabwe kwa miaka dahali mpaka anakaribia kupoteza fahamu na uwezo wa umakini huku akisema bado tena miaka 25??!!

Mungu ndio alipangwa Daud Mwangosi apigwe bomu mbele ya RPC na askari wanne halafu RPC ndio apandishwe cheo??!!

Mungu ndo kapanga alibino wa Tanzania tu wauliwe na kukatwa katwa viungo vyao na binadamu wenzao??!!

Mungu ndo kapanga Tanzania tuwe masikini ili hali katujaalia kila mali asili yenye utajiri??!

Mungu ndo kapanga viongozi wetu baada ya Nyerere wakubuhu kwa wizi na ufisadi huku wakijali tu nepotism??!!

Pasco mkuu najua unajua na unakubali unaabudu brown envelopes,je siku hizi unakula maharage ya wapi??!!

cc Pasco
Usiwe mgumu kukubali. Ni kweli kabisa yote hayo yamepangwa na Mungu. Labda swali liwe ni Mungu yupi maana wako wengi. Kuna Mungu wa ISIS, AlQaeda, Alshabab na Siasa kali yeye Anakunywa damu kila kukicha. Kuna Mungu wa wajapani yeye hakuna kulala ni kazi na kujenga uchumi kwenda mbele. Halafu kuna Mungu wa Watanzania, unafiki wa Mapambio, ibada za uongo na kweli, kufunga mwezi Mzima kinafiki, ngono na miziki ya kishenzi pamoja na ujinga uliokithiri. Huyu ndie anatuamulia marais pamoja na matukio yote uliyoyataja
 
Last edited by a moderator:
nakuunga mkono ,yawezekana kabisa.maana dalili ziko wazi. wengi hasa chamani waliona hana vigezo,japokuwa ni mtendaji mzuri sana lakini kasoro yake moja au mbili za kibinadamu zilimfanya aonekane hafai chamani.ila kwa hapa tulipofika hakuna jinsi,ndiyr anayeweza kuvuka kigingi kigumu cha oct 2015!
 
Kwa ziara alizo zifanya mkuu wa utendaji katika chama, dalili zipo wazi kwamba ndie atakae pewa bendera kuipeperusha..Kuna tathimini imefanywa kuhusu yeye na ushawishi kwa wananchi pamoja na wanachama.

Hii itafanyika ili kunusuru mpasuko maana kila kambi yenye nguvu inakubaliana nae..
 
Usiwe mgumu kukubali. Ni kweli kabisa yote hayo yamepangwa na Mungu. Labda swali liwe ni Mungu yupi maana wako wengi. Kuna Mungu wa ISIS, AlQaeda, Alshabab na Siasa kali yeye Anakunywa damu kila kukicha. Kuna Mungu wa wajapani yeye hakuna kulala ni kazi na kujenga uchumi kwenda mbele. Halafu kuna Mungu wa Watanzania, unafiki wa Mapambio, ibada za uongo na kweli, kufunga mwezi Mzima kinafiki, ngono na miziki ya kishenzi pamoja na ujinga uliokithiri. Huyu ndie anatuamulia marais pamoja na matukio yote uliyoyataja

Ambae ni Mungu wako pia??!!
 
Kwa ziara alizo zifanya mkuu wa utendaji katika chama, dalili zipo wazi kwamba ndie atakae pewa bendera kuipeperusha..Kuna tathimini imefanywa kuhusu yeye na ushawishi kwa wananchi pamoja na wanachama.

Hii itafanyika ili kunusuru mpasuko maana kila kambi yenye nguvu inakubaliana nae..

Dentist himself??!! Kwa usafi upi??!!

Usafi wa ile kampuni yake inayohusishwa na usafirishaji wa Vipusa??!! Jina ni kama Al-Sharaf shipping company.

Kwa usafi wa ile kampuni yake pale TALL??!!

Kwa uadilifu wake wa kugeuza Arusha kimbilio la Wasomali na yeye mwenyewe akiwa ni mwenyeji wa asili ya Somali??!!

Sithani kama hilo linawezekana,kwani PTC,COTEC na wengineo watapinga balaa!!!
 
Then hii thread inakuzidi kimo, bakia kuwa msomaji tu, wenyewe tunaelewana vizuri tu Bonafide genuine.

Mkuu kama kweli sauti ya wengi ndio sauti ya Mungu mbona kauli hii haikudhihirika Shinyanga mjini 2010?
 
Nikusahihishe Pasco. Kuna tofauti kati ya kujua kitakachotokea na kupanga kitakachotokea.

As God exists outside of time, He knows what is to come. That does not mean that He plans it.

Ni kweli Mungu anajua kama tutaweza kuwa na Rais na atakuwa nani. Hiyo haimaanishi Yeye anamchagua huyo mtu.

Mungu hatuchukii. Ametuumba na ruksa ya kuchagua. Tulichagua mtu mbaya kipindi kinachomalizika. Hatatunyima utashi wa kuchagua mtu mbaya tena, yaani Lowasa.

Tumetawaliwa na wezi na wanyanganyi kwa miaka mingi. Tusipobadilisha chama tawala tukachagua fisadi basi atakuwa ni chaguo letu. Sio chaguo la Mungu.
 
JK anaendelea kuwashangaza baadhi ya watu. Yaani kuna watu wanadhani JK anaweza akasimamia jambo gumu mwanzo mwisho. Naomba niwakumbushe kwamba hana historia hiyo. Sifa yake pekee ni kuwa kigeugeu. Huu ni msimamo wa muda tu, mtapigwa na butwaa pale atakapobadili upepo. Sababu za kubadili upepo zipo nyingi, lakin nitazitaja tatu:
  1. Njia inayotumiwa na 'jamaa ya Pasco' na wagombea wengine wa CCM ndiyo aliyoitumia hata yeye. Hivyo hakuna jipya. Na anaweza akaulizwa kwenye vikao kwamba mbona unafunga mlango uliopitia ili wengine wasipite?
  2. Urais ndiyo kitu pekee kinachompa nguvu ya maamuzi ndani ya chama. Lakin urais unaisha mwezi wa 10, baada ya hapo atakuwa wa kawaida, tena kuna watu ndani ya chama watakuwa na nguvu kuliko yeye kwasababu ya mtandao na pesa.
  3. Hulka. Kubadili uelekeo kwa makusudi au bahati mbaya ni jadi ya JK. Hata Mbowe ni shahidi mzuri wa hili maana wakati wa uzinduzi wa bunge la katiba, Mbowe alimpa JK 'standing ovation' huku akipiga meza kwa nguvu sana. Hiyo ilitokea dakika 30 za mwanzo. Mwisho wa hotuba ya JK hautasahaulika kichwani mwa Mbowe.
 
...asa unakataza watu kutaja majina wakati wewe mwenyewe unataja kwa mafumbo, au kutaja kwa mafumbo ni sawa?
 
Back
Top Bottom