Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
jamani hii habari sijaielewa huyu anasema kweli au just ndio fitna zenyewe?
iweje donge wakatae kufanyika mikutano ya siasa hule kwao?
source Michuzi
ZENGWE LA KAMPENI JIMBO LA DONGE

Habari Kaka Michuzi,
natuai humzima na unaendelea vyema na libeneke.naomba uwape wadau hii ili waweze kuchangia maoni yao.
Kulikuwa na tetesi na hatimaye mwaka huu yalirushwa rasmi matangazo katika baadhi ya vituo vya redio na wanaojiita wazee wa jimbo la donge kwamba hawataki mikutano ya kampeni jimboni mwao.
Hali hii imedhihirika jana baada ya viongozi wa CUF kuhitilafiana na kikundi kidogo cha watu walioaminika kuwa wakaazi jirani na eneo ambalo lingefanyika mkutano jumamosi ya leo tarehe 16/10/2010, hivyo mkutano kufutwa ili kuepusha ghasia ambazo zingejitokeza.
Shamhuna amekuwa nyuma ya kikundi kidogo cha wazee hapo jimboni kwake kuzuia demokrasia ikiwa ni pamoja na kura ya maoni iliyofanyika Julai 31 mwaka huu ambapo kura nyingi za hapana zilipatikana kupinga kuwepo na serikali ya kitaifa baada ya uchaguzi oktoba 2010 baada ya kuaminika kupiga kampeni ya kimya kimya.
Mnamo kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, Shamhuna alitumia nafasi yake kama naibu waziri kiongozi na waziri wa habari na utamaduni kuwaamrisha polisi kuzuia wanachama wa upinzani umbali wa maili 6 toka jimboni donge walikokuwa wakienda kuhudhuria mkutano wa kampeni hali iliyosababisha ghasia iliyoleta usumbufu na watu kadhaa kuumizwa.
Tayari viongozi wa upinzani wameanza kutuhumu baadhi ya viongozi waandamizi serikalini kwa kubeza na hatimaye kuuhujumu muafaka uliofikiwa.