Hii ya Azania Bank ni halali kisheria?

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Azan Bank wametoa tangazo hili kwenye Magazeti kuhusu waliokuwa watumishi wa Benki hiyo ambao wameshindwa kulipa mikopo:


Je hii ni halali kisheri kumtangaza mdeni wako kwenye vyombo vya habari ?
 

Attachments

  • AZANIA.jpg
    43.9 KB · Views: 148
Mhh haya mambo ya kuanikana kwenye magazeti ni balaa kwakweli,kwakweli sijui sheria
inasemaje kuhusu hilo,tena ex-staff lol!!
 
Bank linajukumu la kuhakikisha linahifadhi nyaraka zote za mteja wao hata pale atakapo kufa, bank hairuhusiwi kudisclose information za mteja kwa mtu yoyote ILA TU KUTAKAPOKUWA NA SABABU MAALUMU KAMA;
1. KUNA SHERIA INATAKA HIVYO,
2. MTEJA KARUHUSU,
3. KWA MANUFAA YA TAIFA.
4. N.k

ILA UHUSIANO WA BANK NA MTEJA NI UHUSIANO WA KIMKATABA(contractual relationship), hivyo basi uhusiano huu hutawaliwa na makubaliano(ambayo yapo kwenye mkataba) baina ya wahusika, kwenye mikataba kuna kitu kinaitwa mode of communication in case of default yaani mtawasiliana vipi kutakapo tokea tatizo la kimkataba mfano umeshindwa kulipa, na humo huainishwa njia mbali mbali za mawasiliano sasa basi mimi na wewe hatujui kwenye mkataba wa hao ex staff walikubaliana what mode of communication. Labda huko kuanikana kwenye magazeti walikubaliana wenyewe.

Pia sheria inataka itolewe notice kwa muhusika aliyeshindwa kulipa deni ili kumpa muhusika muda wa kujiandaa kulipa deni au kunaweza kukatokea makubaliano baina ya bank na mteja na hivyo kuepusha kufungua kesi ambayo ingeleta mrundikano wa kesi ili hali kumbe mnaweza kukubaliana bila kwenda mahakamani.
 

Nini sijaelewa au? kwani hao ni ex-staff au wateja wa Azania?

Kisheria Azania wanayo haki kufanya walichokifanya for public intrest kama mabenk mengine wanaweza kuingia mkenge kuwakopesa watu wasiokopesheka, taasisi za umma na saccos.

Well done Azania Bank
 
Itakuwa hunanielewa na hujasoma mwanzo hadi mwisho nilichoandika. Go back and read between lines what i have wrote. Unaweza kuwa ex staff au staff na wakati huo huo ukawa mteja wa bank.
 
Azan Bank wametoa tangazo hili kwenye Magazeti kuhusu waliokuwa watumishi wa Benki hiyo ambao wameshindwa kulipa mikopo:



Je hii ni halali kisheri kumtangaza mdeni wako kwenye vyombo vya habari ?

uKIONA HIVYO KUNA MKATABA WENYE HICHO KIPENGELE CHA KUTOA PICHA ZAO KWENYE PUBLIC NA VINGINEVYO WANAVYONA INAFAA BAADA YA MTEJA KUKAIDI.WALE WENYE MCHEZO WA KUTAPELE VYOMBO VYA FEDHA KAENI CHONJO MABENKI YOTE YANA HICHO KIPENGELE TUSIJE KUONA LEO UNAKUNYWA BIA KESHO KWENYE GAZETI.
HERI YA MWAKA MPYA
 
Ukiingia mkataba wa loan na Bank kwa masharti kadhaa ikiwemo kupitisha salary ndio makato yaendelee,pindi uondokapo unatakiwa uende tena kwa mkataba mpya wako ba Bank,usipofuata kama mkataba unavyosema wana haki kukuanika na kukutumia wale wanaidai kwa niaba ya Bank...(Majembe etc)....sheria iko wazi!kalipe usitafute huruma ya JF
 
hata kama uliacha kazi azania kwa nini usipeleke marejesho ya watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…